Waziri wa Habari, Vijana Vijana, Utamaduni na Michezo, Tabia Maulid Mwita amewataka vijana kuzitumia fursa zinazotolewa na Baraza la Vijana Zanzibar kwa lengo la kutatua changamoto mabalimbali zinazowakabili.
Akizindua kampeni ya Program ya Mobile Youth Space (MYS)
na Kampeni ya ’’Amani ni Tunu, Vijana Tuitunzeni’’, Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari,Vijana, tamaduni na Michezo, kwa naiba ya Wizara hiyo Mh Tabia Maulid
Mwita amesema vijana bado wanakabiliwa na changamoto ya ushiriki na
ushirikishwaji hususan katika mambo yanayowahusu na hatimae kukosa fursa na
nafasi mbalimbali katika jamii ikiwemo ajira na uongozi katika ngazi za
maamuzi.
Amesema Sera ya Maendeleo ya vijana ya Zanzibar ya
2013, imeonesha wazi changamoto ya ushiriki na ushirikishwaji wa vijana
katika ngazi za maamuzi, kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo ya Kitaifa
katika Nyanja za kiuchumi, kijamii na kisiasa licha ya jitihada mbalimbali
zinazochukuliwa.
“ Ushiriki wenye tija kwa vijana ni nguzo sahihi ya
upatikanaji wa taarifa zinzowahusu na hatimae kuleta tija iliokusudiwa’’,
Waziri Tabia.
Amesema Programa hiyo itatekelezwa kupitia mikutano ya wazi (Public meeting) inalenga kuwafikia vijana 39,600 katika Wilaya zote za Unguja na Pemba na kujumuisha shughuli mbali mbaliza utoaji elimu kwa wananchi kupitia vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii na vipeperushi.
Mapema Katibu Mtendaji wa Baraza la Vijana Zanzibar, Ali Haji amesema vijana wana nafasi kubwa ya kulinda tunu ya Amani na utulivu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025, kuijiunga katika mabaraza ya vijana bila kujali itikadi ya vyama kwa lengo la kunufaika na fursa zinazotolewa na pamoja na kulinda Amani ya nchi.
“Mabaraza ya vijana ni yenu, naomba muyatumie ili
kueleza changamoto zenu na kujiletea maendeleo”, Ali Haji, Katibu Mtendaji,
Baraza la Vijana Zanzibar.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi kutoka Kijij cha kulelea watoto yatima Zanzibar (SOS )Gharib Abdalla Hamad amesema shirika hilo ni wadau wakubwa wa maendeleo ya vijana hivyo wataendelea kuunga mkono juhudi za wizara hiyo ili kuweza kufikiwa kwa maendeleo bora ya vijana hapa nchini.
Program ya MYS inatarajiwa kutekelezwa na Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, kupitia Baraza la Vijana kwa kushirikiana
na Shirika la SOS kwa kipindi cha miaka 3, kutoka April 2025 hadi April 2028,
iliobeba ujumbe ’’ USHIRIKI NA USHIRIKISHWASJI NA UPATIKANAJI WA
TAARIFA SAHIHI KWA VIJANA NI MSINGI WA MAENDELEO ENDELEVU’’.
0 Comments