NA AMRAT KOMBO, ZANZIBAR:
SIKU zote baadhi ya watu wanaimani ya kuwa, mwanamke bado ni mama wa nyumbani pekee.
Ambae anatakiwa kuchunga familia yake tu peke yake, lakini bila ya kufikiri kuwa mwanamke anaweza kufanya mambo makubwa ya kuwasaidia jamii na kuleta maendeleo katika nchi.
Ushahidi wa hili, sasa usiangalia tena Marekani na kwengineko, njoo kwa Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania, alivokuwa jasiri na mchapa kazi, katika nafasi yake ya uwongozi.
Hivyo inaonesha kuwa, mwanamke sio mdhaifu kama watu wanavoona, hebu tuangalie baadhi ya viongozi wanamke wanavyowajibika katika nafasi zao.
Fatma Rashid Juma ni diwani wa Chukwani Unguja, amesema kabla ya kushika nafasi hiyo, alikuwa mfanya biashara mjasiria mali mdogo, huku akiwa mwanancha wa chama cha mapinduzi CCM.
Amesema katika mwaka 2020, alijishirikisha katika kugombea udiwani wakiwa na wagombea wenzake 11, wakiwa wanawake watatu na wanaume nane, na kubahatika kutokea mshindi kwenye kinyanganyiro hicho kwa kupata kura 49 katika watu 100.
Sababu iliyopelekea kuingia katika siasa, amesema zipo nyingi ingawa moja ni kutetea haki za wanyonge, kuweza kupaza sauti zao.
Licha ya hayo amesema uongozi hauna umri kila mtu anahaki ya kusimamia na kutetea, na hasa akishafikia ule umri wa kuanza kupiga kura.
Diwani Fatma amefanya mambo mbali mbali ambayo yameweza kuwasaidia wananchi wake, ikiwemo kutengeneza barabara ya kijiji cha Shakani na ya Chukwani, kutengenezea banda la wajasiria mali 20 katika skuli ya Chukwani, lenye gharama ya shiling 5,700,000 na kwasasa anapambana kutengeneza kituo cha daladala cha Chukwani.
Ukiachia na hayo anatarajia kutengeneza kisima katika wadi ya Chukwani na Buyu, ili kuona wananchi wake wanaondokana na changamoto ya maji.
Vikwanzo ambavyo amepitia wakati alipopata nafasi ya uwongozi ikiwemo baadhi ya wagombea wenzake kuwepo kwa matabaka, lakini alifanikiwa kukabiliana na vikwazo hivyo kwa kuamua kujishusha chini na kuanza kuwasikiliza maoni yao.
"Wakati nilipopata hii nafasi, nilipata changamoto mbalimbali ikiwrmo wagombea wenzangu, kuweka matabaka pamoja na maneno yasio kwisha, ingawa niliamua kupambana na changamoto hiyo na kufanikiwa kuishinda,’’amesemaFatma
Barke Juma ambae anamfahamu diwani huyo amesema amepata kiongozi imara mwenye utu, ambae anasaidia kutatua changamoto zinazowakabili kwenye wadi yao.
Hamadi Makame, amesema wamepata kiongozi anaewajibika katika majukumu yake, na ataendelea kumuunga mkono, ili aweze kufanya kazi kwa wepesi.
Sheha wa Chukwani Suleiman Mohamed Mwinyi, amesema kuna umuhimu wa kuwepo viongozi wanawake kama Diwani Fatma, kwani wanakuwa na ushawishi mkubwa katika uwongozi wao.
"Haswa wanapopewa mafunzo, huwa mstari wa mbele katika kufahamu mambo mengi, wanakuwa waaminifu katika uwongozi wao kama alivyo diwani wetu,’’amesema Suleiman
Anaona viongozi walio wengi wanawake, wamekuwa watetezi wakubwa katika shughuli mbali mbali, ikiwemo katika sekta ya kupiga vita vitendo vya ukali na udhalilishaji.
Katika wadi yao amesema wametoa viongozi mbalimbali wanawake kwa lengo la kuwajengea uwezo na kusimamia maendeleo ya shehia hiyo.
"Katika shehia yetu, tunao viongozi wanawake, kwa mfano tumewahi kuwa na mbunge mwanamke, diwani mwanamke hadi kufikia mwenyekiti wa halimashauri wa wilaya, na akanzisha vikundi tofauti vya maendeleo,’’amesema Suleiman
"Kwasasa tuna mkuu wa wilaya mwanamke ambae ni mchakarikaji, mshumpavu, na mwenye kuvumilia kero za wananchi, pamoja na kutatua changamoto zetu, akishirikiana na diwani Fatma,’’ameeleza.
Licha ya yote hayo amesema diwani Fatma amefanya jitihada mbalimbali za kimaendeleo, ikiwemo kuhamasisha masuala ya afya, kiuchumi pamoja na kufanya ubunifu wa kueka banda la ujasiria mali kwa lengo la kuweza kujikwamua na umaskini.
Mkurugenzi wa Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar - ZAFELA Jamila Mohammed amesema wanatoa elimu mbalimbali, kwa wanawake ambao wanahitaji kuwa kiongozi, ili wajitambue na kutatua changamoto za kiuongozi.
"Na hii inawapa hamasa na kuweza kutambua haki zao za kidemokrasia, siasa, mila na utamaduni ikiwemo haki ya kupata elimu, afya pamoja na miundombinu,’’amesema Jamila
Mkurugenzi Jamila amesema hadi sasa zaidi ya wanawake 172 wamepatiwa mafunzo ya uwongozi kutoka Unguja na Pemba, pamoja na kutambua vikwazo na namna ya kukabiliana navyo.
Aidha amewanasihi wanawake wanaotaka kuingia kwenye uongozi kutokuwa na hofu, kama Katiba inavyosema katika serikali zote mbili inavyoelezea pamoja na mikataba mbalimbali ya kitaifa na kikanda.
Mkurugezi wa Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Thabit Idarous Faina, amesema hali halisi ya viongozi wanawake Zanzibar, kupitia nafasi ya uwakilishi kwenye majimbo 50, ya Zanzibar wanawake ni wanane pekee.
"Wabunge wanaowakilisha Zanzibar wanawake ni wanne tu sawa na asilimia nane, huku mawaziri wakiwa sita sawa na asilimia 33 na makatibu wakuu ni saba sawa na asilimia 39 , na kwa upande wa wakuu wa mikoa, mwanamke ni moja tu sawa na asilimia 20,wakuu wa wilaya ni wanane sawa na asilimia 36 na masheha wanawake ni 68 sawa na asilimia 17 kwa masheha wote ambao ni 389"
Amesema miongoni mwa vikwanzo vya wanawake kutoingia kwenye uwongozi, ikiwemo majukwaa ya kisiasa yanatajwa kuwa ni moja wapo ya vikwanzo vinavyosababisha wanawake wasifikie malengo yao.
0 Comments