NA FAUZIA MUSSA
Kaimu Mkurugenzi Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano WA Afrika Mashariki OFISI ya zanzibar, Balozi Silima Kombo Haji , amesema ujio wa wajumbe wa nchi mbalimbali kunatoa fursa za utalii na uwekezaji nchiini.
akizungumza na sheikh el Amin Omer el Amin kutoka Sudan aliyefika Ofisini kwake maisara kujitambulisha alitumia fursa hiyo kumkaribisha kutembelea maeneo mbalimbali ya Zanzibar kujionea fursa za uwekezaji zilizopo katika Kisiwa hicho.
Balozi Kombo alimweleza Sheikh El Amin kuwa kwa sasa vipaombele vya uwekezaji ndani ya Zanzibar ni biashara ya utalii, viwanda na uchumi wa Buluu na kumshauri kufika Mamlaka ya uwekezaji na kukuza uchumi ZIPA Ili kupata maelezo zaidi ya maeneo ambayo yapo tayari kuwekezwa.
Alifafanua kuwa uchumi wa Buluu umekusanya masuala ya Uvuvi WA bahari kuu, utalii wa bahari kupitia visiwa vidogo vidogo, mafuta na gesi, Pamoja na usafirishaji wa baharini,
Alibainisha kuwa watanzania na wasudani ni ndugu wa Muda mrefu hivyo kuja kuwekeza katika Kisiwa cha Zanzibar kutaimarisha zaidi undugu wao.
Kwa upande wake sheikh El Amin Omer El Amin alisema ni mara ya Kwanza kufika Zanzibar lakini amevutiwa na nchi hiyo na wananchi wake kutokana na ukarimu na ustaarabu waliyonao hasa kwa wageni wanaoingia Nchini.
Alisema kabla ya kufika katika nchi hiyo alisikia sifa mbalimbali zinazotajwa kuwepo na kuzithibitisha baada ya kutembelea ambapo kwa Sasa anatamani kuwa sehemu ya Zanzibar.
Sheikh El Amin alisema ni wazi zanzibar ina vivutio vingi na maeneo mbalimbali ya uwekezaji na kusema kuwa yupo tayari kuwekeza katika maeneo ya utalii Ili kukamilisha dhamira Yake ya kuwa sehemu ya Zanzibar.
Sheikh El Amin, ni msudan anayeishi Nchini Uiengereza ambae amefika Zanzibar Pamoja na mambo mengine lakini pia ana lengo la kutafuta maeneo ya uwekezaji kupitia utalii visiwani Zanzibar .
0 Comments