NA
FAUZIA MUSSA:
Mkurugenzi Idara ya
Elimu na Maandalizi, Fatma Mode Ramadhan, amewataka walimu kuthamini juhudi za
wadau wa maendeleo wanaosaidia kuimarisha miundombinu ya elimu ili kuwa na
mazingira mazuri ya kufundisha na kujifunzia.
Wito huo aliutoa
wakati akizungumza na walimu wa skuli ya maandalizi Jang’ombe katika hafla ya makabidhiano
ya ujenzi wa sakafu nje ya skuli hiyo chini ya ufadhili wa Taasisi ya KOICA Tanzania kupitia mradi wa kuimarisha mazingira ya watoto ya kujifunzia.
Alisema juhudi
zinazofanywa na Taasisi hiyo zinaakisi maono ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi katika kuimarisha sekta ya elimu
nchini na zinaimarisha mashirikiano yaliopo kati ya Zanzibar na Korea na kusema
kuwa Serikali inawakaribisha wadau wengine kuwekeza kwa watoto wa maandalizi na
msingi kwani ndio Taifa la kesho.
Alieleza kuwa
maboresho hayo yanawapa hamasa wanafunzi kuendelea kujifunza kutokana na kuwa
na eneo salama la kujifunza na kuchezea ikiwa ni sehemu ya kuimarisha hali ya
elimu kwa watoto hao.
“kuweka mazingira
mazuri ya kujifunzia kunaongeza ujuzi wa watoto wetu na kunaimarisha afya zao kimwili
na kiakili” Alisema
Mkurugenzi huyo aliwashukuru
KOICA kwa msaada wao katika unaoimarisha hali ya elimu ya maandalizi ikiwa nipamoja
na kuweka miundombinu ya elimu, vifaa vya kujifunzia na kufundushia na
kuwaongezea ujuzi walimu wa wanafunzi hao.
Mkurugenzi wa KOICA
Tanzania, Manshik Shin aliishukuru Wizara ya elimu Kwa mashirikiano yao na Taasisi
hiyo na kuahidi kuendelea kuisaidia Tanzania Zanzibar kadiri hali
itakavyoruhusu ili kuhakikisha wanafunzi wanakua katakia mazingira bora ya
kujifunzia.
Alieleza kuwa
kukamilika kwa mradi huo kutasaaidia kuongeza ubora wa elimu kutokana na
kuwasaidia walimu kufanya kazi vizuri na kuongeza mbinu mpya za kufundushia.
Akitoa maelezo ya
mradi huo Nakyoung lel wa KOICA Tanzani alisema hatua hiyo ilitokana na kuwa
eneo hilo halikua rafiki kwa wanafunzi na kuwa katika hatari ya kuumia wakati
wowote hali iliyowakosesha hamu ya kusoma na kutohudhuria skuliipasavyo hasa
kipindi cha mvua.
Alibainisha kuwa
mradi huo ulilenga kutatua kero na adha zilizokuwepo awali na kusema kuwa wamefanikiwa
kwa kiasi kikubwa kwani kumekuwa na ongezeko la watoto wanaohudhuria skuli kwa wakati
wote bila kujali hali ya hewa.
Alifahamisha kuwa
mradi huo ulihusisha kuweka sakafu nje ya skuli hiyo ukarabati wa vyoo, kuchora
picha katika kuta, kuweka maua pamoja na ujenzi wa miteremko na kingo ili
kuzuia hatari ya wanafunzi kuanguka zoezi lililoanza Oktoba mwaka huu.
Mwalimu Mkuu wa
skuli hiyo Harusi Mbarouk Khamis, aliishukuru Wizara ya elimu kwa kuwapokea wahisani
hao waliosaidia kuwapatia mazingira mazuri ya kufundishia pamoja na vifaa
vinavyotoa hamasa kwa watoto kujifunza.
Mwalim Harusi
aliahidi kutunza eneo hilo ili kuenda sambamba na dira ya skuli inayoelekeza
kuwa na skuli bora yenye mazingira mazuri ya kufundisha na kujifunzia.
Alibainisha kuwa
awali wanafunzi wao walipata athari kutokana na kujichoma na mawe yaliyokuwepo eneo
hilo na baadhi ya wakati kuanguka kutokana na kuteleza na kusema kuwa hatua
hiyo imeondoa changamoto hiyo na kuwa sasa watoto wao watasoma bila udhia.
0 Comments