Na-Thuwaiba Habibu.
Inaweza ikawa sawa na nyimbo yenye vibwagizo vizuri vya kuvutia kuhusu uongozi na wanawake ila nyimbo hizo ambavyo wadau na wanaharakati wanaimba juu ya wanawake kupewa nafasi kuwa viongozi kibwagizo chake ni kigumu kuitikia pale wimbo huo unaposikika ,
Aisha Haji Mzee 25,mama wa mtoto mmoja mkaazi wa Kisauni Unguja ambaye aligombea nafasi ya uwakilishi mwaka 2020 wakati huo akiwa na umri wa 21.
Aisha ambaye aligombea nafasi hio kupitia Chama cha ADA TADEA,amesema kwamba ushirikiano kutoka kwa ndugu wa karibu ulikuwa ni mdogo hii ni kwa sababu ya kuwa aligombea chama pinzani .
"Baba yangu alikuwa hataki mimi niingie katika siasa katika chama tofauti na yeye hakuwa na mashirikiano kwa ninachokifanya ilifika hatua hadi nikaondoka nyumbani" Amesema Aisha.
Kutokuungwa mkono huko hakuharibu tu mahusiano yake na familia ila bado pia ndoa yake ilipitia magumu pia.
"Nilivyoanza kujishugulisha na siasa tafrani za kwenye ndoa zikaanza na ikafika wakati mume wangu pia akaniacha niliumia na kurudi nyuma zaidi”.
Amesema Aisha huku akionesha kuwa ameumia kuhusu suala hilo.Wapo watu ambao waliojitoa kwa ajili ya kumsaidia Aisha kama ambavyo Mwenyekiti wa Chama pamoja na mama yake kwa sababu wao waliamini kuwa hizo ni ndoto zake na ana haki ya kuzipambani
"Mama alinambia pambana na ndoto zako usisikilize watu kwani unachokitaka ndio sahihi kwa upande wako.” Amemaliza Aisha.
Asiata Said Abubakar kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA ambaye alijiunga na chama hicho mwaka 1994 akiwa huko Mkoa wa Kilimanjaro Mwaka 2006 aligombea nafasi za muweka hazina ndani ya chama kwa upande wa Kanda ya Unguja nafasi ambayo naishikilia hadi sasa. Akiwa bado ameshikia nafasi ya muweka hazina ,mwaka 2014 aligombea nafasi ya Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake –BAWACHA Jimbo la Kikwajuni.
Asiata amesema kuwa mila na desturi zinanakwamisha wanawake kuingia katika uongozi maana familia bado zina imani ile ile ya dhana potofu juu ya wanawake.
"Baadhi ya familia wanaon fursa za wanawake kuwa viongozi na ikitokea akaweza akajitokeza mwanamke wa kufanya hivyo atawekewa vikwazo ili ashindwe kama mimi mume wangu aliniacha sababu ni ya kuingia kwenye siasa na kutaka uongozi " Amesema Asiata.
Rahma Mussa nae pia alikumbana na changamoto katika familia yake zilizotaka kukwamisha malengo yake ya kuwa kiongozi. Rahma 25 ambaye kwa ni Katibu wa UVCCM tawi la Jitipopo kupitia Chama Cha Mapinduzi mwaka 2018 ambaye ndoto zake ni kuwa kiongozi.
”Kuna watu wanatawaliwa na mfumo dume na kuamini wanawake sio sehemu ya utawala katika jamii bali ni wakutawaaliwa tu"
Amesema Rahima ambaye anaona kuwa jamii inahitaji zaidi elimu ya kuwashika mkono wanawake
"Jamii lazima itowe mashirikiano kwa wanawake ya kuwaongezea nguvu wanapoamua kuingia kwenye Uongozi kwani wanauwezo wa kuleta mabadiliko katika nchi" Amemaliza Rahima.
Suala la kuungwa mkono na familia,jamii na hata viongozi wa vyama ni changamoto inawakumba wanawake,Naibu Katibu wa Chama cha ACT WAZALENDO Zanzibar, Omari Ali Shehe amesema ipo haja ya kuelimisha jamii na kubadilisha mitazamo ya kuelewa kuwa wanawake wana haki ya kushiriki nafasi za uongozi kama ambavyo inatokea kwa wanaume.
”Sisi Chama chetu tunatoa mafunzo kwa wanajamii na tunashukuru wanaume ameaanza kuelewa" Amesema Omar huku akitoa wito kuwa"Tuachane tabia ya kumuona mwanamke hana uwezo wowote bali tutoe fursa na mashirikiano ili tuone mchango wao".
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Chama cha ADA TADEA,Ali Makame Issa amekiri kuwa kuna baadhi wanaume hawataki wake zao kuwa viongozi kutokana na makubaliano wanayojiwekea baina yao wawili.
"Wapo baadhi ya wanaume hawataki wake zao kuwa viongozi na hata kufanya kazi za serikalini na ikitokea mmoja akavunja makubaliano ndio hutengana na ndoa kuvunjika" Amesema Ali.
Sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2022 inaonesha Zanzibar ina watu 1,889,773 kati ya hao wanaume ni 915 ,492 huku wanawake ni 974 ,281 hii ikimanisha wanawake ni wengi.
Wanaharaki wa masuala ya wanawake wamekuwa mstari wa mbele kuwasaidia wanawake kuweza kujitokeza na kupambania ndoto zao kama anavyofanya Mkurugenzi wa chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania -Tamwa DKt Mzuri Issa amesema muda mrefu wanawake wamekua na nafasi ndogo katika uongozi hususan kwenye ngazi za maamuzi na ndio maana waliamua kuwajengea uwezo na kuwashajiisha watumie fursa ziliopo kugombea uongozi.
"Tunashajihisha wanawake kuingia katika uongozi ili kupata wakilishi wa matatizo ya wanawake wenzao” Amesema Maryam.
Serikali ikiwa sehemu ya juhudi hizi Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Anna Atanas Paul amesema atashangaa sana kusikia kama bado kuna familia zinamuona mwanamke ni mtu duni hasa Zanzibar.
"Kama zipo familia zinazofanya hivyo ziondokane na dhana hizo kwani taifa linakuwa kukiwa na mashirikiano kwa jinsia zote utazidi kuona uwezo wa wanawake katika uongozi na kuleta Mabadiliko"
Amesema Naibu Waziri Anna huku akizitaka jamii kuwa kutoa fursa sawa baina jinsi zote mbili kwani ni mwanamke ni muhimu sana kuwepo katika kila setka zote ili watoe mchango wao na kusaidia jamii.
Kwa mujibu wa Itifaki ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC ambayo mkataba wake ulitiwa saini mwaka 2008 inaeleza kutaka kuondoa utofauti na kuwatenga wanawake katika nyanja mbalimbali za maendeleo na kusaidia kuwepo usawa wa kijinsia katika nchi wanachama na kufikia asilimia 50/50 kwenye maamuzi, serikali na taasisi binafsi.
0 Comments