Ofisa
michezo kutoka idara ya michezo chini ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, Saleh Hashim, akizungumza wakati akizindua ligi ya mchezo ya kabaddi
muhula wa kwanza katika viwanja vya New Amaani Compex.
NA FAUZIA MUSSA:
Katika kuadhimisha
miaka minne ya Dk. Mwinyi, shirikisho la kabadi Zanzibar limeandaa ligi ya
mchezo huo msimu wa kwanza ambapo kufanyika kwa mashindano hayo kutasaidia
kuutangaza mchezo huo ndani ya jamii.
Hayo yameelezwa na
ofisa michezo kutoka idara ya michezo chini ya Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Saleh Hashim wakati akizindua mashindano hayo
yatakayodumu kwa siku tano katika viwanja vya New Amaani Compex.
Alisema uzowefu
unaonesha kuwa mchezo huo bado ni mgeni kwa jamii hivyo aliwaomba vijana
kujifunza kupitia mashindano hayo.
Alieleza kuwa Wizara
inafarajika kuona michezo mbalimbali inaongezeka hali inayosaidia kuitangaza
nchi na kusema kuwa wizara itaendelea kuchukua juhudi za makusudi kuhakikisha
mchezo huo unatambulika na kuendelezwa.
Alifahamisha kuwa
hatua hiyo pia inaonesha wazi maendeleo ya mchezo huo ulioanzishwa miaka miwili
iliyopita, na kuwaomba wadau wa michezo kuongeza nguvu katika mchezo huo ili
kuupa thamani na kuutambulisha kwa watu.
Mkurugenzi wa
maendeleo ya michezo wa shirikisho la chama cha kabadi Zanzibar, Abdalla Juma
Abeid na Makamu Mwenyekiti wa mchezo huo, Ali Seif Juma, walisema historia
inaandikwa kwa kuzindua mashindano hayo kwani haijawahi kufanyika tangu kuanza
kuchezwa kwa mchezo huo visiwani Zanzibar.
Walieleza kuwa
kuimarika na kuongezeka kwa michezo kunaenda sambamba na juhudi za Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi Dk. Hussein
Ali Mwinyi za kuwekeza
katika sekta ya michezo, na kusema kuwa ligi hiyo ni maalum kwaajili ya
kumpongeza kiongozi huyo kwa mageuzia makubwa aliyoyafanya katika sekta ya
michezo.
Walifahamisha kuwa
timu 12 zitashiriki katika michuano ya mchezo huo zikiwemo timu nne za wanawake
ambapo mara baada ya ufunguzi timu ya
KMKM wanawake
watachuana na Lumumba wanawake, na kwa upande wa wanaume timu ya KMKM na
Lumumba zitapimana nguvu.
Viongozi hao
walilishukuru Baraza la michezo kupitia Wizara ya Habari kwa msaada wao
uliyofanikisha michuano hiyo Kufanyika katika viwanja hivyo na kusema kwao ni
fursa ya kuutangaza.
Naifat Ame Hassan na
Samir Mubarak Sururu wa timu ya kabadi KMKM walisema wanatarajia kupata ubingwa
katika ligi hiyo kwani suala hilo sio geni kwao na wameshafanikiwa katika
michezo mingi iliyopita na kupata vikombe.
Aidha wachezaji hao
waliahidi kutomwangusha Dk. Mwinyi kwa kuiwakilisha vyema nchi wanaposhiriki
mchezo huo ndani na nje ya nchi.
Adam Makame Hamad na
Sina Mussa wa timu ya kabadi Lumumba walimshukuru Rais wa Zanziba na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi kwa mchango wake unaosaidia kuitambulisha michezo
mbalimbali ikiwemo kabadi na kuwashauri vijana kujiunga na mchezo huo kwani
utawasiadia kuwatoa kimaisha, na kuimarisha afya zao.
Watazamaji wa michuano
hiyo akiwemo Ahlam Khamis walionesha kufurahishwa na mchezo huo na kusema kuwa
wanatamani kujiunga.
Michuano hiyo
inakwenda sambamba na kauli mbiu “ miaka minne ya Dk. Hussein
kabadi inajieleza”
0 Comments