Ticker

6/recent/ticker-posts

Wadau Wa Mabadiliko Ya Tabia Ya Nchi Kukutana Zanzibar Oktoba 20 Hadi 22


Na Nihifadhi Issa Na Ahmed Abdulla:

CHAMA cha waandishi wa habari Wanawake  TAMWA ZNZ kwa kushirikiana na wadau wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ikiwemo Taasisi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi (ZACCA) na Afisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar, imeandaa mkutano wa kwanza wa mabadiliko ya tabianchi utakaofanyika Zanzibar

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari huko Tunguu Ofisi za TAMWA Mwenyekiti wa kamati ya Jukwaa la mabadiliko ya tabianchi Zanzibar.(ZANCCC) Mahfudh Shaban Haji, amesema lengo la mkutano huo ni kujenga uwezo, uelewa na hamasa kwa asasi za kiraia, wanajamii na Idara za Serikali kufahamu dhana nzima ya mabadiliko ya tabianchi na athari zake

Ameeleza kuwa katika mkutano huo mikakati mbali mbali ya kitaifa na kimataifa, ikiwemo mkakati wa mabadiliko ya tabia nchi wa mwaka 2024, sera na mkakati wa uchumi wa buluu, uwajibikaji na matumizi sahihi ya rasilimali za nchi itajadiliwa

‘'Tunafahamu  kuwa mabadiliko ya Tabianchi ni suala mtambuka mkutano utaainisha lengo hili la maendeleo endelevu la 23 na malengo mengine 16 yaliyokusudiwa  kupitia vipindi na mada mbali mbali’’ amesema  Mahfudh.

Aidha ameongeza ili kuipa nguvu kauli ya Zanzibar ya kijani ni vyema jitihada za ziada kuchukuliwa pamoja na kutoa elimu kwa jamii umuhimu wa  utunzaji  mazingira. 

Kwa upande wake  Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wahabari Wanawake TAMWA ZNZ Dkt Mzuri Issa amewataka waandishi wa habari kuandika habari zinazoibua changamoto za mabadiliko ya tabianchi ili ziweze kuwafikia walengwa na kufanyiwa kazi.

‘’waandishi wahabari tumieni kalamu zenu kuyaibua na kuyafanyia uchechemuzi masuala ya mabadiliko ya tabianchi kwa upana wake pamoja na kuzungumza athari wanazopata wanawake kupitia mabadiliko hayo’’ Dkt Mzuri Issa TAMWA ZNZ.

Kwa upande wake mwakilishi wa Taasisi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ZACCA Ngwali O. Ngwali amesema Ukataji wa mikoko unachochea zaidi Mabadiliko ya tabia nchi katika maeneo ya fukwe za bahari miongoni mwao ni Mkokotoni,fungurefu na Donge na Charawe kuwa yameathirika kwa kiasi kikubwa na 

Mkutano huo wenye kauli mbiu 'imarisha uhimili wa mabadiliko ya tabianchi Zanzibar '' utakaofanyika Oktoba 20 hadi 22 katika Ukumbi wa Idrissa Abdulwakil Kikwajuni  unaotarajiwa kufunguliwa na Waziri wa Afisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na  Jumla ya washiriki 250 kutoka ndani na nje Zanzibar wanahudhuria.

Post a Comment

0 Comments