Katibu Mkuu Wizara ya
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi Abeida Rashid Abdallah amesema Miongozo
na Sera inayohusu Watu Wenye Ulemavu kwa sasa haitosherelezi hivyo ipo haja ya kuangalia
Sera na Sheria zingine namna ilivyowajumuisha Watu Wenye Ulemavu ili
kuhakikisha kwamba hakuna kundi ambalo limeachwa nyuma katika jamiii.
Ameyasema hayo mwishoni
mwa wiki iliyopita wakati akifungua mkutano wa programu
ya Kimataifa ya Haki za Watu Wenye Ulemavu, uliyofanyika katika ukumbi wa
Goden Tulip, Uwanja wa Ndege, Unguja.
Amesema Sera ya mwaka 2004 inayohusu Watu Wenye Ulemavu haitosherelezi
hivyo ipo haja ya kuangalia Sera na sheria zingine namna ilivyowajumuisha Watu Wenye
Ulemavu. Alieza kama hakuna basi Watu Wenye Ulemavu wanalazimika kupaza
sauti zao kwa kuwaambia jamii changamoto zinazowakabili kutokana na mapungufu yaliyopo kwenya Sera na
Sheria iliyopo.
"Miongozo na Sera ya 2004
ambayo inawajumuisha Watu Wenye Ulemavu ipo ambapo kupitia programu hii ya kikao cha leo inafanyiwa
review hivyo lazima tushukuru. Lakini pale ambayo tunaona mapungufu lazima tuwaoneshe
wenzetu nini tunahitaji” Alisema bi Abeida.
Aidha bi Abeida amesema
muda sio mrefu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto
itazindua Mpango Kazi wa Kitaifa wa
Kumpambana na vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto ambapo Mpango huo
umezingatia masuala ya Watu Wenye Ulemavu.
Pia alitoa wito kwa Watu
Wenye Ulemavu kuweka takwimu zao ingawa Serikali inaweka lakini ni vyema na wao
wenyewe kuweka takwimu zao vizuri ili ziweze kuwasaidia wakati wa kutoa maoni
yao.
Mwisho Bi Abeida
amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suhuhu Hassan na
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinnyi kwa uongozi wao
pamoja na kuzingatia masuala ya Usawa wa Kijinsia na masuala ya Watu Wenye Ulemavu.
Mapema akizungumza Mtaalamu
wa Ushauri masuala ya Usawa wa Kijinsia bi Maja Hansen Amesema mkutano huo wa
Haki za Watu Wenye Ulemavu umelenga kuzungmzia ajenda nne ikiwemo Ushiriki na
Ushirikishaji, Ulinzi wa vitendo vya ukatili kwa Watu Wenye Ulemavu, Maboresho ya Sera, na Masuala
ya takwimu ambapo anaamini mkutao huo
utaleta tija.
Kwa upande wa washiriki wa Mkutano huo, akizungumza Ali Omar Makame kutoka Shirikisho la Jumuiya la Watu Wenye Ulemavu Zanzibar (SHIJUWAZA) amesema amefurahishwa na hatua ya waandaji wa mkutano huo walivyowashirikisha Watu Wenye Ulemavu katika kikao hicho, kwani wataweza kueleza changamoto zinazowakabili ikiwemo ukosefu wa vyoo rafiki kwa baadhi ya majengo ya Serikali na Binafsi.
0 Comments