Bodi ya ligi Tanzania bara imetua ratiba ya ligi kuu soka
Tanzania Bara ambapo miamba ya soka Tanzania Simba Na Yanga imepangwa kukutana
Oktobar 19, 2024 katika Dimba la KMC majira ya Saa 11: za jioni.
Miamba hiyo itakuwa ni mara ya pili kukutana kwa msimu huu
ambapo mara ya kwanzi ilikutana Agosti 08, 2024 kwenye mchezo wa ngao ya jamii
na Yanga kupata ushindi wa 1-0 lililopachikwa kimiani na Kiungo mshambuliaji
Max Nzingeli mnamo dakika ya 44.
Kwenye ligi kuu msimo uliopita Yanga ilipata ushindi katika
michezo yote miwili ambapo mchezo wa awali walishinda 5-1 huku mchezo wa pili
ikipata ushindi wa 2-1.
0 Comments