Ticker

6/recent/ticker-posts

Sheria,Sera Za Vyama Vya Siasa Kurekebishwa Kuzuia Unyanyasaji Wa Wanawake Kwenye Siasa

 


Naibu Msajili wa vyama vya siasa Mohammed Ali Ahmed amesema sheria na kanuni za maadili ya vyama vya siasa zinaendelea  kufanyiwa marekebisho kwa lengo la kuweka usawa wa kijinsia pamoja na kukuza uwajibikaji na kuzuia unyanyasaji dhidi ya wanawake ili waweza kushiriki kikamilifu katika siasa na  demokrasia nchini.

Akizungumza kwa niaba ya Naibu Msajili wa vyama vya siasa, Afisa sheria Mwandamizi kutoka ofisi hiyo Abdulrazak Ali kwenye mkutano wa tathmini iliyoangalia vikwazo vinavyowakwaza wanawake katika kugombea na kushiriki masuala ya kisiasa  uliofanyika  ukumbi wa ZURA Maisara mjini Unguja, ambao uliowashirikisha wadau mbalimbali kutoka taasisi za Serikali, vyama vya siasa, Asasi za kiraia, wanaharakati na viongozi wa dini.

Akizitaja sheria na kanuni zinazoendelea kufanyiwa marekebisho ni pamoja na Political Parties Act (2019), Political Parties Code of Conduct (CAP.258 R.E.2019), Regulation of 2019, na Kanuni za maadili ya vyama vya siasa na kanuni nyenginezo, marekebisho hayo  yatakapo kamilika yanatarajiwa  kuondoa unyanyasaji kwa wanawake katika kushiriki masuala ya kisiasa.

Afisa sheria mwandamizi, alisisitiza kuwa usawa wa kijinsia ni jambo lisilopingika, hivyo ni muhimu kwa vyama vya siasa kuzingatia hilo kwa kuandaa miongozo imara  itakayosimamia maadili na kukemea vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wanawake, sambamba na kuunga mkono wanasiasa wanawake, wagombea, wapiga kura ambao wanaweza kukabili vitisho, vurugu, kashfa na dhihaka kutokana na jinsia zao katika kuwania nafasi mbalimbali za uongozi.

Mapema akimkaribisha Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, na Watoto, Mkurugenzi wa TAMWA Zanzibar Dkt Mzuri Issa amesema kumekuwa na malalamiko ya wanawake kudhalilishwa wakiwa katika haraki za ushiriki wao katika siasa na hakuna mifumo mizuri ya kuripoti matukio hayo na upatikanaji wa haki

Nae Naibu Waziri  wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee, na Watoto Mhe Anna Athanas Paul,  amesema Wizara hiyo imeandaa mikakati maalum ikiwemo kutoa mafunzo, nyenzo na programu za ushauri ili kusaidia wagombea wanawake.

Tathmini ya vikwazo kwa wanawake katika kushiriki kwenye  siasa na demokrasia imefanywa na TAMWA Zanzibar  kwa kushirikiana na Shirika la Kitaifa la Kidemokrasia (NDI) na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID).

Post a Comment

0 Comments