Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi la
Zanzibar,Mgeni Hassan Juma ameishauri
taasisi za serikali na za kiraia kujitahidi kubuni mifumo itakayosaidia
kuongeza idadi ya wanawake katika nafasi za uongozi.
Akizungumza
na mwaandishi wa gazeti hili nyumbani kwake Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja
amesema ni vyema tasisi za serikali
pamoja na za umma kuwapatia wanawake
fursa ya viongozi ili kusaidia katika
harakati zake za kimaendeleo.
Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mgeni Hassan
Juma alisema wanawake wachangamkiee nafasi za uongozi ili9 kutetea haki na
maslahi yao na watoto, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto, Siti Abbas Ali anasikitika kuendelea kwa utamaduni wa jamii kuona uongozi
ni fursa inayomfaa tu mwanamme na kusahau kuwa hata mwanamke ametokana na Adam
Na Hawa, kama historia inavoelekeza.
Naibu Spika Mgeni aliyehojiwa akiwa nyumbani kwake
Tunguu, nje kidogo ya jiji la Zanzibar, amesema matatizo mbalimbali
yanayomkabili mwanamke na watoto yanaelekea kumhitaji sana kiongozi mwanamke
ambaye haraka hupata hisia kali anapoyaona na hubakiwa na mzigo wa athari
yakishatokea.
Bi Mgeni anasema mwanamke akipata uongozi imani
hujengeka kwamba huwa mstari wa mbele kupigania maslahi ya mwanamke na mtoto
katika nchi akitoa mfano wa tatizo linalokua la udhalilishaji.
Hata hivyo, analalamika kuwepo mazingira yanayokwaza
wanawake kupata nafasi za uongozi hivyo wachache mno kufanikiwa kupenya.
"Muamko wa wanawake kushiriki kutafuta uongozi
ni mdogo kutokana na hofu, vitisho na
dhana potofu.
"Tunakutana na changamoto nyingi
zinazotukwamisha kuingia kwenye uongozi. Mtu unashindwa kugombea jimbo kutokana
na ugumu wa kupambana na mwanamme. Hili jambo si rahisi kwetu wanawake,"
anasema.
Anasema kwa upande mwengine ni haki ya kikatiba
mwanamke kuwa kiongozi na kwamba akiingia humsaidia kunufaika kiuchumi na
kuendeleza familia yake.
"Tunahitaji mabadiliko. Angalia hapa petu
Zanzibar kwa sababu ya mfumo mbaya, katika majimbo 50 ya uchaguzi, tunao wawakilishi
wanane tu waliochaguliwa majimboni. Utadhani hakuna wanawake majimboni au labda
hawataki. Hapana. Wanahofia mapambano na wanaume," alisema.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na
Watoto, Bi Siti anasema,
"Kwenye shehia zetu kunaanzishwa kamati tofauti
kuhusu afya, mazingira, elimu masuala yanayohusu kila mtu lakini utakuta
wajumbe wengi ni wanaume kama vile Shehia haina wanawake wenye uwezo.
"Baadhi ya changamoto zinazokwamisha wanawake
kugombea jimboni ni mtu kuona atashindwa tu maana atapambana na mwanamme na
mitazamo ya wananchi ni kuamini zaidi wanaume katika uongozi kuliko wanawake.
"Wanawake wengi ndio wapiga kura, tukisimama
kwa pamoja katika kumnyanyua mwanamke itasaidia wengi kushika nafasi lakini
mfumo waliotujengea wazee wetu kuona mwanamme ndo anapaswa kuwa kiongozi
tunakwama."
Kwa kuliona hilo, Wizara yetu hujenga njia ya
kuhamasisha wananchi katika sekta mbalimbali ikiwemo kutambua na kuzidai haki
zao, katika ajira, elimu ya uongozi."
Mkurugenzi wa Uchaguzi Zanzibar ( ZEC), Thabit
Idarous Faina amesema hali halisi ya viongozi wanawake Zanzibar kupitia nafasi
ya uwakilishi kwenye majimbo 50 ya Zanzibar ni idadi ya mawaziri sita katika
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, sawa na asilimia 33, makatibu wakuu ni saba
ambayo ni sawa na asilimia 39.
Kuhusu wakuu wa mikoa, alisema yupo mwanamke mmoja
tu, ikiwa ni sawa na asilimia 20; wakuu wa wilaya wapo wanane ambayo ni sawa na
asilimia 36 na Masheha 389 waliopo nchi nzima, 68 tu ndio wanawake ambayo ni
asilimia 17.
Ametaja vikwazo vinavyozuia mwanamke kuingia kusaka
uongozi ni pamoja na woga wa mwanamke na zile hatua ngumu za kupita mpaka
kufikia kuwa kiongozi wa wananchi.
0 Comments