Ticker

6/recent/ticker-posts

Kazi 161 Uhamasishaji Wa Upatikanaji Wa Sheria Mpya Na Rafiki Za Habari Zawasilishwa

 


Na Ahmed Abdulla na Amrat Kombo

Jumla ya kazi za waandishi wa habari 161 zinazotoa ushawishi juu ya upatikanaji wa sheria mpya ya habari Visiwani Zanzibar zimeandikwa na kurushwa katika vyombo vya habari tofauti ikiwemo radio, televisheni,mitandao ya kijamii  na magazeti kwa kipindi cha mwaka mmoja kutoka mwejzi Julai 2023 hadi Juni 2024.

Akiwasilisha mrejesho wa kazi kwa niaba ya afisa  ufatiliaji na tathimini Khairat Haji alisema hiyo ni baada ya waandishi wa habari 25  kutoka Unguja na Pemba kupatiwa mafunzo ya na namna bora ya kufanya ushawishi kwenye taarifa zao wanazoziandika kwa lengo la kupata sheria Mpya ya habari itakayopanua uhuru wa waandishi wa habari na vyombo vya habari.

alisema mrejesho huo unaonesha kuwa waandishi 15  kutoka Unguja walipatiwa elimu hiyo na chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania Upande wa Zanzibar TAMWA-ZNZ ni waandishi wa habari 10 tu ndio  walifanikiwa  kutoa mrejesho  wa kazi walizofanya  ambazo ziliweza kutoa maoni tofauti katika vichwa vya watu.

Afisa mratibu wa sheria za habari Zaina Mzee alisema ikiwa ni mwaka  wa pili sasa katika kuhamasisha upatikanaji wa sheria mpya ya habari lakini sheria hiyo haijapatikana licha mwanga kuanza kuonekana.

“Tulishakutana na viongozi mbalimbali  kujadili jambo hili kwa jumla ni mikutano mitano ambayo ilifanywa na wadau wa habari  (ZAMECO) wakiwa na tume ya kurekebisha sheria ,tume ya utangazaji, viongozi wa baraza la wawakilishi na viongozi wengine lakini bado halijapata muwafaka” alisema Zaina.

Aidha alisema sheria ya habari iliyo rafiki pekee ndio inayoweza kuiheshimisha tasnia ya habari hivyo  wadau wa habari wanatakiwa kuongeza nguvu ya ushawishi wa upatikanaji wa sheria mpya na rafiki ya habari ili kuona inajitengemea na haingiliwi na mamlaka yoyote kwani kinyume na  hivyo kunakosesha uhuru wa kujieleza na kutoa taarifa.

Mjumbe wa bodi wa chama cha waandishi wa habari  wanawake Tanzania Upande wa Zanzibar TAMWA-ZNZ Hawra Shamte aliwataka waandishi kuendelea  kutumia kalamu zao kuhakikisha sheria ya habari  rafiki inapatikana

Bi Hawra aliendelea kusisitiza kuwa “tunategemea sheria zetu zitatoka kwa makatibu wakuu na kuacha kupigwa dana dana kutokana na ahadi tunazopewa kwa sheria zetu kuu mbili za habari ikiwa ni wakala wa usajili magazeti, na tume ya utangazaji kwa sababu tushazisemea sana na tunazidi kuziandikia  hadi tuone mafanikio”

Kwa upande wake muandishi wa habari mkongwe Salim Said Salim aliwaomba waandishi  kutokata tamaa  na kuendelea  kuandika na kusemezea sheria hizo mpaka kufikia malengo.

Pia alisema “Tunatakiwa kuandikia stori au makala zitakazoonesha  mifano ya nchi waliofanikiwa kuwa na sheria a habari rafiki kama Kenya  na Uganda ili kuleta hamasa zaidi ya kupatiwa sheria mpya”.

Nao baadhi ya mwaandishi  waliopatiwa mafunzo hayo walisema wataendele kuandika habari zinazohusu mapungufu ya sheria za sasa za habari kwasababu lengo halijatimia kwani waandishi wa habari ni  moja ya wahanga wa mkandamizo wa sheria hizo

“Tukipata sheria rafiki itakuwa rahisi kwetu kupata taarifa bila vikwazo” walieleza

Post a Comment

0 Comments