Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi,Alhaj
Dkt. Hussein Ali Mwinyi Leo Jumamosi Julai 20, 2024 amejumuika pamoja na
Viongozi Wakuu, Masheikh, na Waumini mbali mbali wa Kiislamu, katika Maziko ya
Bi. Zuleikha bint Ahmad ambaye ni mama Mzazi wa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira
wa Wavu Zanzibar (ZAVA) Kassim Haidar.
Marehemu amesaliwa Msikiti wa Ijumaa Malindi, ambapo Sala imeongozwa na Mtoto wake, Sheikh
Ahmad Haidar na kuzikwa katika Makaburi ya hapo hapo Msikitini, Mkoa wa
Mjini-Magharibi, Unguja.
Viongozi wengine wa Serikali, Dini na Jamii wamehudhuria
Maziko hayo ikiwa ni pamoja na Makamu wa kwanza Wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Alhaj Othman Massoud Othman, Makamu wa Pili wa Rais Alhaj Hemed Suleiman
Abdulla, Spika wa baraza la Wawakilishi Zanzibar Zubeir Ali Maulid na Mufti
mkuu wa Zanzibar Saleh Omar Kabi.
Mwenyezi Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi,
Amiin!
Innalillahi Waina Ilayhi Raajiun!
0 Comments