Na Najjat Omar,Zanzibar:
Ni saa nne asubuhi Warda amekaa kwenye meza ya kulia na kaka zake watatu wakiwa wanakunywa chai hapa nyumbani kwao Mtoni Wilaya ya Mjini .Mkoa wa Mjini Magharib.
Hapa ni nyumbani kwao kwa mama yake Mkasi Abdallah na baba yake Masoud Ali, Warda akiwa ni mtoto wa mwisho mwenye umri wa miaka 7 anasoma darasa la pili anapenda kucheza mpira akiwa na kaka zake.Ni kawaida na ni mtindo wao wa maisha baada ya kurudi skuli jioni huungana na kaka zake kucheza mpira kwenye sehemu ya uwa wa nyumba yao.
Maisha ya aina hii yamemfanya Warda kupenda kuwa mchezaji mpira hata hushiriki kucheza mpira akiwa skuli, jambo la kukuza kipaji chake si suala ambalo lilipo kwa mama yake maana haoni sababu ya binti yake kuwa mwanamichezo hususan ukizingatia anaamini kuwa mpira wa miguu sio sehemu ya maisha ya wanawake.
“Naona anapenda kucheza na ni kwa sababu ya kaka zake ila kama wangekuwa wanawake wawili asingekuwa anacheza mpira” Amesema Mkasi akiendelea kusema ,ndoto zake kwa Warda ni awe daktari na sio mchezaji mpira.”Anacheza kama sehemu ya mchezo wa kitoto la hawezi na sisi hatuwezi kumuacha acheze mpira baba yake hataki na mimi sikubali hilo” Amemaliza Mkasi.
Mwandishi wa Makala hii aliomba ruhusa ya kuzungumza na Warda na alipopewa nafasi alitamani kujua juu ya uchezaji wake wa mpira. “Kaka zangu wanacheza na mimi wananifundisha na skuli mimi ni kipa kwenye timu yetu nataka kucheza niende Simba Queen huko Dar “amesema Warda huku akitabasamu.
Masuala ya kidini yatarudisha juhudi za kuwa kucheza mpira wa miguu kutokana na Imani ya kwamba mchezo huu sio wa wanawaume kama ambavyo Warda anavyosema “Baba anasema pia huu sio mchezo wa Wanawake na pia nguo za kuchezea mpira ni suruali mama hataki “amesema Warda.
Ni dhahiri kwamba ndoto za kuichezea Simba Queen inaweza kufa kuanzia sasa huku kipaji alichonacho kisiwe na muendelezo wa kuendelea.Huku familia yake itasimamia kuhakikisha Warda wanazifukia ndoto hizi ambazo zinakinzana na mila,tamaduni na hata Imani ya dini ya Kiislam.
Utafiti wa Taasis ya Wanawake kwenye michezo nchini Marekani (Women’s Sport Foundation) inaonesha kwamba wasichana ambao wana umri wa miaka 14 huacha kuendelea na michezo ikiwa tofauti na wavulana kwenye umri huo huo kuendelea kwenye michezo.
Utafiti huo unaonesha kuwa hamasa katika familia inakosekana ndio sababu kubwa ya wasichana kuacha michezo huku karibu wasichana milioni 1.3 hushiriki michezo wakiwa skuli kati ya umri wa miaka 5 hadi 13.
Huku kati hao milioni 1.3 ni asilimia 43 tu ndio huanza michezo wakiwa skuli na kujiona wanamichezo, asilimia 68 wanakuwa na hofu ya kuhukumiwa kuwa kwenye michezo,asilimia 61 wanakuwa na hofu ya kuwa na ujasiri ,huku asilimia 47 wakipata msukumo wa kuendelea na masomo ya skuli na asilimia 43 wanahisi hawako salama kushiriki kwenye michezo.
Riziki Islah ni Kocha na muwezeshaji wa masuala ya kimichezo amethubutu kuvunja miiko hio na kuwasaidia wasichana kuwasaidia kucheza na kujikita zaidi kwenye michezo.” Sio tu kwa Warda tu la familia nyingi haziamini kwenye kucheza mpira na hio ndio sababu mimi niliacha kucheza na kuanza kuwasaidia wasichana kama mkufunzi na mwalimu kwenye michezo na hio imeongeza ushawishi wa jamii kuona nilikuwa mwanamichezo na sasa ni mwalimu nikiwa mwanamke” Ameendelea kusema kuwa michezo kwake ni sehemu ya maisha kwani imempa fursa nyingi sana”Mimi nimefika hadi marekani kwa sababu ya michezo ni vyema hizi dhana ziachwe kwenye familia na watoto wasaidiwe kucheza mpira” Amemaliza Riziki.
Neema Machano ni Katibu wa soka la Wanawake hapa visiwani Zanzibar licha ya kuwa mchezaji mpira anakiri kuwepo kwa dhana ya uhuni kwenye michezo kwa wasichana “Uhuni ni dhana tu,ila malezi ndio husabibisha tabia za kuhuni ila michezo ni ajira na maisha kuzuia vipaji kwa wasichana kama dhana ya uhuni si sahihi” Amesema Neema.
Mhadhir Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu Cha Taifa Cha Zanzibar Suza Profesa Issa Ziddy amesema kiuhalisia michezo ni matendo au mazoezi ya kimwili ambayo mara nyingi yana ushindani ndani yake na inaelezwa kuwa michezo ina umuhimu mkubwa kwa ukuwaji,ustawi amesema suala na familia kusisitisha kutokuwaruhusu ni kutokana na mwingiliano wa Wanawake na wanaume na ubadilishaji wa tabia wa Watoto Wanawake “Dini haijakataza ila imekemea ile hali ya wanaume na Wanawake ni vyema Wanawake wawe na Wanawake wenzao kwenye michezo hapo inaswihi” Amesema Profesa Ziddy.
0 Comments