Na Najjat Omar:
Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ambayo ni 17 kati ya hayo lengo namba 5 linazungumzia “Usawa wa Jinsia” hii ina maana ya ushirikishwaji na ushirikiano kwenye kufanikisha usawa wa jinsia kwa upande wa wanaume na wavulana na wanawake na wasichana.
Mei 24, Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi alipokea ugeni kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ambapo amesema kuwa anashukuru Zanzibar kuwa mmoja ya waandaaji wa Mashindano ya African Football Championship mwaka huu hii ikiwa ni hatua muhimu sana kwenye seka ya michezo visiwani Zanzibar.
Kupitia Bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar ya mwaka 2024/2025, Waziri wa Elimu Lela Muhamed Mussa aliesema kwa mwaka huo kutakuwa imarishwaji wa miundonmbinu ya Elimu kwa kujenga madarasa 1500 kupitia ujenzi wa Skuli za Ghorofa, Skuli za Chini na kukamilisha madarasa yaliyoanzishwa na wananchi, kwa Unguja na Pemba.
Katika juhudi za ujenzi wa skuli nzuri za ghorofa ila kumekuwepo kwa uhaba wa viwanja vya michezo ambavyo vimechukuliwa na ujenzi wa skuli hizo kwa kuwa sehemu ya bustani na hata kuwepo kwa ukuta mkubwa ambao unaweka mandhari nzuri wa skuli hizo.
Skui ya Msingi Bububu “A” na Sekondari Ali Hassan Mwinyi iliyopo Bububu Wilaya Mjini Magharib imekosa viwanja vya michezo licha ya moja wapo kuwa ya ghorofa huku ujenzi wa madarasa mazuri,sehemu ya kuegeshea gari,na ukumbi wa sherehe ila skuli hii haina sehemu maalum au hata kiwanja cha mchezo wa aina yoyote ndani yake.
Nusrat Ali Kombo 16, ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza hapa amesema hakuna mazingira ya kimichezo ni mara moja moja sana ndio wanafunzi wanaume huzunguka nje ya skuli kucheza mpira” Hakuna sehemu ya michezo mimi napenda kucheza netball ila hapa hakuna kiwanja wakati wa mapumziko tunakula na kukaa kuzungumza tu “Amemaliza Nusrat.
Mwandishi wa Makala hii alizunguka nyuma ya skuli ya Sekondari Ali Hassan Mwinyi na kuona kiwanja ambacho wanafunzi wa kiume hucheza mpira wakati wakiwa na mashindani au muda wa mapumziko, kiwanja ambacho kina michanga huku upande wa pili kukiwa na jaa kubwa la takataka sio salama na kipo karibu na makaazi ya watu.
Akiwa amemaliza kidato cha nne mwaka 2022 kwenye skuli hii Hamad Issa amemaliza mazoezi hapo anavua viatu yake vya mazoezi na kushika mkononi anasema kukosekana na viwanja wa michezo kwenye skuli ni jambo ambalo linaua vipaji “Skuli nzuri mimi nimesoma hapa ila haina sehemu ya michezo hii si nzuri ” Amesema Hamad huku akiendelea na safari yake ya kurudi nyumbani akiwa na wenzake wanne.
Taarifa ya uandikishaji wa wanafunzi skuli za msingi mwaka 2022 ambao wanaweza kushiriki michezo ni zaidi ya 300,000 huku kwa mujibu wa ripoti ya Bajeti kwa mwaka 2022/2023 jumla ya wanafunzi 343 wenye vipaji vya michezo ndio wanashiriki michezo mbali mbali katika ngazi ya Kitaifa.
Skuli ya Msingi ya Salim Turky iliyopo Mpendae ni miongoni wa skuli ambazo zimefanyiwa ukaratabi wa kujengwa kwa ghorofa huku skuli hio ikiwa na kiwanja kimoja tu cha kucheza mchezo kikapu ambapo kiwanja hicho wanatumia wanafunzi wa kiume kucheza mpira wakati wa mapumziko.
Kukiwa na michezo mengine wanafunzi hulazimika kutoka nje ya skuli na kuomba kiwanja kilichopo pembezoni wa skuli ili kucheza mpira wa wavu au wa miguu jambo hili linawarudisha nyuma shauku ya wasichana na wavulana wa skuli hii kupenda na kuendeleza michezo.
Ni saa 4:12 za asubuhi huu ni muda wa mapumziko sasa,wavulana wamechukua mpira wao na wanacheza mpira wa miguu kwenye kiwanja hiki kidogo wakiwa na furaha na mabishano nilimuuliza mmoja wao amejitambulisha kwa jina la Abdul-wahid Kassim Issa anasoma darasa la 5 anajiskiaje kucheza mpira “Tunacheza hapa na mimi napenda kucheza mpira mapumziko wakiisha tunarudi darasa”Alimaliza na kurudi kuendelea kucheza. Kitu cha tofauti hapa wasichana wao wamejitenga wako pembeni mwa bustani n acini ya miti wanazungumza inaonesha michezo si suala linawajia kichwani.
Mei 24,2025 Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kupitia Waziri wa Elimu Lela Muhamed Mussa amewasilisha Bajeti ya Wizara ya Elimu kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kwenye kikao cha 8 Mkutano wa 15 wa Baraza la Wakilishi la 10 . Akichangia Bajeti ya Wizara hio Mwakilishi wa Jimbo la Mtambwe Dkt Mohammed Ali Suleiman amesema kuwa ni vyema serikali iangalie miundombinu ya michezo pale wanapojenga skuli za ghorofa “Serikali iangalie uwepo wa viwanja vya michezo kwenye skuli ambazo zinajengwa wa mfumo wa ghorofa ili kuendelea kuwepo wa michezo katika Skuli” Amesema Dkt Mohammed alipokuwa kichangia bajeti hio.
Akiendelea kuchangia juu ya Bajeti hio Haji Shaaban Waziri Mwakilishi wa Jimbo la Uzini amesema miaka ya nyuma kulikuwa na michezo ya aina zote kwenye skuli ila kwa sasa hali hio inapotea na hapo ndipo vipaji vinapoibuliwa “Ni vizuri kutambua kuwa michezo sio burudani tu ila sasa michezo ni ajira niwatake Wizara ione umuhimu wa kurudisha michezo skuli” Amemaliza uchangia.
Hija Mohamed Ramadhani ni Mshauri wa masuala ya jinsia kwenye Mradi wa michezo na Maendeleo unaotekelezwa na Shirika la Maendeleo la Ujerumani amesema mradi huo unapanga kuboresha viwanja 7 vya michezo Visiwani Zanzibar maana Unguja na Pemba ili kutoa fursa za uhamasishaji wa michezo kwa wasichana na wanawake.Ameishauri serikali pia iangalie jinsi ambavyo itasaidia kuwepo kwa viwanja vya michezo katika skuli”Ni vyema kuwepo kwa viwanja ili vipaji viwe na muendelezo na ushawishi katika jamii hivyo ni serikali iangalie hili wakati inapojenga na kufanya ukarabati kwenye skuli “Amemalizia Hija .
0 Comments