NA AMRAT KOMBO,ZANZIBAR
WANAWAKE na
uongozi, wanawake wanaweza bila ya kuwezeshwa, wanawake ni wajasiri, wanawake
ndio wenye uchungu wa maendeleo.
Baada ya
mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi yaliyotokea mwanzoni mwa miaka ya 1990
-ukijumuisha na Mkutano wa Beijing kuhusu uwezeshwaji wa wanawake, taratibu
kibao kilianza kugeuka.
Kwanza,
kuruhusiwa mfumo wa vyama vingi kulimaarisha kutanuka kwa wigo wa wanawake
kuwania nafasi za uongozi kupitia vyama vingine vya kisiasa.
Zaidi ya
chama tawala cha CCM, wanawake sasa walijitokeza kuwania nafasi katika
vyama vya upinzani na kupata fursa ambazo zisingekuwa rahisi kuzipata katika
mfumo wa chama kimoja.
Kuruhusiwa
kwa asasi za kiraia pia kulifungua njia kwa wanawake kuonyesha uwezo, maono na
ujasiri wao kwenye kuhoji na kuishauri serikali kwenye mambo ya maslahi kwa
taifa.
Wanawake
mashuhuri wa miaka ya 1990 kama vile Leila Sheikh Khatib, Dk. Ananilea Nkya,
Mary Rusimbi, Marie Shaba na wengine walipata umaarufu na heshima si kwa
kutumia vyama vya siasa bali zaidi kupitia harakati zao kupitia asasi za
kiraia.
Kama kuna
jambo walilofanikiwa kulifanya wakati ule ilikuwa kuonyesha kwamba wanawake
wanaweza kuwa viongozi pasipo kuwa wanasiasa kamili.
Matokeo yake
ni kwamba mwaka 2010, Tanzania iliweza kupata wanawake wabunge 23 waliopata
nafasi zao kupitia majimbo ya uchaguzi. Ukijumuisha na wale wa viti maalumu,
Bunge la Tanzania likafikisha asilimia 29 ya wabunge wanawake -kiwango cha juu
kabisa kwa wakati huo.
Katika
Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, wanawake wamejitokeza kwa wingi kuwania nafasi
mbalimbali za kuchaguliwa kuanzia Urais, ubunge na udiwani.
Chama cha
upinzani cha ADC kimempitisha mwanamama Queen Sendiga kuwa mgombea wake wa
nafasi ya urais katika uchaguzi huo.
Chama kikuu
cha upinzani kimetangaza orodha ya wagombea wake wa ubunge ambako takribani
wanawake 35 wamejitokeza kwenda majimboni kuwania ubunge. Idadi hiyo ni zaidi
kidogo ya asilimia 20 na ndiyo kiwango kikubwa cha wagombea wanawake kupitishwa
na chama hicho kuwania ubunge tangu kuanzishwa kwake..
Kwa upande wa Zanzibar ,wakati anaingia Ikulu
raisi mstafu DKAli Mohmmed Shein mwaka 2010 alianza kwa kuwapa wanawake nafasi za uwaziri.
Maana wengi
walishaota mizizi kwenye akili zao kwamba, wanawake hawapaswi kuonekana kwenye
meza refu wakiwa mawiziri.
Kwa
miaka mingi tunaona idadi ya wanawake viongozi inaongezeka taratibu kutokana na
mitazamo mbali mbali na juhudi zinazochukuliwa, wapo ambao wanaishia njiani kwa
sababu tofauti lakini wapo ambao wanapambana hadi kuwa viongozi wa majimbo.
Kauli mbiu ya
wanawake na uongozi wakati huo na sasa imeshikiwa bango na wanaharakati kama
vile TAMWA, ZAFELA, ZSLC, TGNP, ZAWCO, na mradi wa WEZA na ndio maana idadi ya
wanaoibukia majimboni inaongezeka.
Na dhamira hii ya mwanamke kupambana inawavutia wengi na wanaamua kuiga mifano yao hadi na wao kutimiza ndoto zao.
Mwakilishi
Mstaafu wa jimbo la Magomeni Hapsa Said Khamis amesema ameingia katika siasa
katika kipindi cha mfumo wa vyama vingi mwaka 1995 lakini hakuwahi kukataa
tamaa .
"
Sikuwa na hofu wakati nagombania kwasababu nilipata ushirikiano katika kijiji
changu kuanzai wazee hadi vijana na nikafanikiwa kushinda miaka yote
miwili." alisema
Pia amesema imani ya mtu ndio inayomsabishia
mtu kufikia malengo yake.
"
Ukiwajengea watu imani wakuamini basi shirikiana nao katika hali yoyote ile
itawafanya kuwa na upendo na wewe." alisema hapsa
Samabamba na
hayo amelezea mbinu mbalimbali ambazo
zitamsaidia mwanamke kuwakiongozi katika jimbo .
"
Kwanza unatakiwa ujitambuwe,uwe na ushirikiano na vyama vyote sio chakwako
tu,kila moja uwoneshe unavomjali, ugonvi hautakiwi ,pamoja kuwathamini wazee
bila ya kuwajali wazee unaweza kupata mitihani." alisema
Wanawake wengi ni wavumiilivu na
wastamilivu,hawajawahi kukata tamaa katika maisha yao,kwa lengo la kuamini kuwa
iko siku wataweza kufanikiwa. Licha ya kuwa kuna baadhi ya watu hujitokeza
katika maisha ya mtu kwa lengo la kumuharibia maisha yake.
Moja kati ya
mwanamke aliyejitokeza kugombea nafasi ya uwongonzi kwa miaka nne
mfululizo lakini hakuweza kufanikiwa .
Hasni Abeid
wa chama cha ACT wazalendo amesema ameanza kugombania tangu 2005 lakini
hakuweza kufanikiwa.
"
Nilipambana na changamoto mbalimbali ikiwemo vitisho lakini niliendelea
kupambana japo haikuwa riski kuweza kushinda nikaendelea kugombea tena
uwakilishi 2010 sikuweza kufanikiwa," alisema
"sikuchoka
nikagombea tena 2015 sikufanikiwa,na siku kata tamaa 2020 nikagombea tena
vilevile sikufanikiwa." aliongezea
Moja kati ya
vijana aliyepatiwa mafunzo na chama cha
uwandishi wa habari wanawake TAMWA
-Zanzibar ,Maimuna Kassimu Yussuf amesema baada ya kupewa mafunzo na chama
hicho alifanikiwa kupata nafasi mbalimbali za uwongozi .
" Elimu
niliyoipata kutoka tamwa imenisaidia kushika nafasi mbalimbali ikiwemo kuwa
mjumbe katika chama cha mpira wa miguu wilaya ya kati,"alisema
"nikaendelea
kupambana tena katika kamati ya uchaguzi wa kamati ya maendeleo shehia ya
kowani nikafanikiwa kuwa mjumbe wa pili. " alisema
Pia amewasaa
vijana wenzake kuendelea kupambana kugombania nafasi za uwongozi kwa lengo la
kujinua kiuchumi.
Lakini
licha ya yote hayo kuna mtazamo kwamba mwanamke hawezi kuwa kiongozi kwa
misingi ya dini ya kiislamu na hivyo kuwafanya baadhi ya wanawake washindwe
Kwenda kwenye majimbo na kugombea.
Amina
Salum Khalifan ni kiongozi wa dini je anazungumziaje suala hilo?.
"Hakuna
dini yoyote iliyokataza mwanamke kuwa kiongonzi tukiangalia katika enzi za
Mtume Muhamma (SAW) tunaambiwa kuwa sio tu alishirikiana na wanawake katika
uongozi, bali aliwapa nafasi ya
kuongoza, hata katika mapigano ya kusimamisha dini ya Kiislamu." alisema
Sambamba na
hayo alisema kuna miongoni mwa wanawake walio shikilia nyadhifa za umma au
nyadhifa kubwa katika karne ya mwanzo na
ya pili Hijria, na kushirikiana na mtume.
"Mwanamke
wa mwanzo aliyeshika na kukubaliwa wadhifa wa ushauri kwa Mtume (SAW) alikuwa
mama yetu mkubwa, Sayyidatuna Khadija binti Khuwayld (Radhiya llahu Anhu)
ambaye alikuwa mshauri wake mkuu kwa hali na mali hata siku moja, Mtume (SAW)
hakuwahi kuukataa ushauri wake." alisema
Mchungaji wa
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Shukuru Malonda, alisema
mwanamke ana nafasi ya uongozi katika kanisa na kijamii na kutoa mfano wa
viongozi wa kike.
Pia amesema waliongoza na kuwasimamia watu
katika dini ya Kikirsto.Miongoni mwao ni Esta ambae alikuwa Malkia na Debora
alikuwa Nabii.
"Katika
kanisa letu tumewachaguwa wanawake wawili
na wanaume wanne ambao ni
wachungaji na Wainjilist 12, wanawake
watano na wanaume saba, ndio wanaoongoza kanisa," alisema.
Mkurugenzi
wa Uchaguzi Zanzibar ( ZEC), Thabit Idarous Faina amesema hali halisi ya
viongozi wanawake Zanzibar kupitia nafasi ya uwakilishi kwenye majimbo 50 ya
Zanzibar ni idadi ya mawaziri sita katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, sawa
na asilimia 33, makatibu wakuu ni saba ambayo ni sawa na asilimia 39.
Kuhusu wakuu
wa mikoa, alisema yupo mwanamke mmoja tu, ikiwa ni sawa na asilimia 20 ,wakuu
wa wilaya wapo wanane ambayo ni sawa na asilimia 36 na Masheha 389 waliopo nchi
nzima, 68 tu ndio wanawake ambayo ni asilimia 17.
Katika mwaka
1964 wabunge wanawake walikuwa 3 hadi
sasa wabunge wanawake wako 148 sawa asilimia 37.7 ya wabunge wote 390 walioko
sasa.
Leo hii kati ya mihimili mitatu ya dola,wanawake wanaongoza mihimili miwili, Serikali na bunge jambo linalothibitisha kuendelea kuimarika kwa usawa na kijinsia.
0 Comments