Mradi wa ujenzi wa Maegesho ya Gari Michamvi |
Na Ahmed Abdulla, Zanzibar:
Mapambano ya
kuhakikisha wanawake anafikia lengo la kuwa kiongozi kwenye ngazi mbalimbali
bado yanaendelea.
Hii inatokana na
matumaini kwa jumuiya zisizo za kiserikali zinazopigania usawa wa kijinsia kwenye
uongozi na demokrasi visiwani Zanzibar kuona mwanga wa mafanikio juu ya nafasi
ya mwanamke kwenye eneo hilo.
Moja ya maeneo ambayo
yameanza kuleta mwanga ni baraza la madiwani Wilaya ya kusini.
Baraza hilo lina
wajumbe nane, sita kati yao wakiwa ni wanawake na wawili wakiwa ni wanaume.
Lakini uwepo wa idadi
kubwa kwenye baraza hilo inaleta faida gani kwa baraza hilo na wananchi wa
Wilaya hiyo?
Mwenyekiti wa Baraza
hilo Mustafa Mohammed Haji ambaye pia ni Diwani wa wadi ya Muyuni alisema madiwani
wanawake kumekuw na mchango mkubwa katika kuibua miradi mbalimbali ya
kimaendeleo ikiwemo Kiwanja cha Kufurahishia watoto kinachoendelea kujengwa
Paje, Stebi ya Magari Michamvi pamoja na Masoko yaliyojengwa maeneo mbalimbali.
“Wanawake hawa
wamekuwa mstari wa mbele katika katika kuchangia mikakati ya kuona tunapata
fedha za kukidhi mahitaji ya miradi ambayo tumejipangia kwenye Bajeti ya mwaka
husika” Alisema
Vilevile Mwenyekiti
huyo alisema madiwani wanawake wa baraza hilo wamekuwa wafuatiliaji wakubwa wa
utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kuzingatia muda na ubora wa miradi hiyo.
“kamati nyinyi za
baraza kuna madiwani wanawake kwa hivyo ule uharaka wao wa kuwaelekeza
watendaji wafikekwenye eneo la Mradi inawafanya hata watendaji wawe na kasi ya
uwajibikaji kwenye miradi hiyi” Aliongeza
Zawadi Hamdu Vuai ni diwani
wa wadi ya Kiongoni, alisema wanawake ni
binadamu kama walivyo wanaume na
wanamudu majukumu yote ya kiungozi katika maeneo wanayoongoza kwa kutekeleza
miradi ya maendeleo inayolenga kuwanufaisha wananchi wanaowaongoza sambamba na
kuleta ukombozi wa jamii zao.
“Jamii humtegemea kila
mwenye uwezo, wanawake tunao uwezo mkubwa hasa kwenye usimamizi wa fedha za
umma zinazolenga kujenga miradi” Alisema Diwani huyo
Aidha alisema suala la
kuwa mwanamke anaweza kuongoza ama laa ni suala la kuangalia utendaji wa
viongozi wanawake kwani matendo na matokeo chanya ya viongozi wanawake
yanaonekana huku akiwataka wenye mtazamo kuwa wanamke hawezi kuongoza waondoe
mtazamo huo.
Mda Mohammed Shaka ni
Diwani wa kuteuliwa Wilaya ya Kusini yeye alisema kazi za kiutendaji ndio
hizohizo wanazozifanya wanaume na wanazitekeleza kikamilifu ama zaidi ya hao
wanaume huku akiiomba jamii kundoa hofu juu ya kuongozwa na mwanamke.
“Tunauwezo sawa au
hata kuwashinda hao wanaume kwenye utendanji” Alisema
Upande wa diwani wa
Viti Maalum Wilaya Ya Kusini Maulid Hassan Zidi alisema lengo lao ni
kuibadilisha Halmashauri ya Wilaya ya kusini Kuwa Manispaa.
“Tunataka kuipeleka
Halmashauri kuwa Manispaa na tunaamini kutokana na miradi tunayotekeleza kwa
sasa tutafanikisha hilo” alisema
Kwa msingi huo
inaonyesha kuwa wanawake wanaweza kuongoza endapo wataaminiwa na kupewa nafasi.
Hivyo ni jukumu la
kila mmoja kwa nafasi yake anaanza kumuandaa mwanamke kiuongozi hata akiwa
mtoto mdogo.
0 Comments