Uongozi ni wajibu kwa kila mtu ikiwa mwanaume au mwanamke
hata kundi la watoto wakiwa wakike au wakiume wanaweza kuwa viongozi kwa aina
yao na sehemu waliyo ndani ya jamii zao.
Lakini wanaume warika mbalimbali wamekuwa ndio waongozaji katika sekta
mbalimbali kuliko wanawake, na hii kutokana na
mtazamo finyu wa jamii kuona mwanaume ndio anaepaswa kuwa kiongozi .
Uongozi nini ?
Uwongozi ni mamlaka ya kuwaonyesha watu njia kwa vitendo.
Vilevile uongozi ni jinsi gani kiongozi anaweza kuleta
ushawishi kwa watu na kufikia maendeleo yaliyotarajiwa.
Kuna aina njia nyingi
za kuainisha uongozi lakini njia ya msingi ni kuangalia jinsi kiongozi
alivyoingia madarakani na utaratibu wake wa kuongoza.
Katika viongozi wapo Wafalme, Maraisi, Mawaziri, Watemi,
Machifu, Wakurugenzi, Viongozi wa dini.
Viongozi wanawake ni wachache katika sehemu mbalimbali
ikiwemo mashuleni hadi katika tasisi mbalimbali. Nahii kutokana na mfumo dume
uliowekwa tangu enzi za ukoloni.
Hali hii inawafanya wanawake wengi kukosa elimu,urithi,
nafasi za uwongozi na kuwa na sauti
iliyosikika na kuheshimika katika kufanya maamuzi.
Raisi Mstaafu wa Skuli ya Bembelela Zanzibar Lelam Abdallah
Twaha alisema sababu zinazopelekea wanaume kuwa wengi katika sehemu ya uwongozi
katika kazi tofauti ikiwemo ya
maskulini.
" Wanaume kutotaka kuongonzwa na wanawake,vilevile
wanawake kuogopa kujitokeza katika nafasi za kugombea, baadhi ya walimu kupenda
mwanaume ndio awe kiongozi."
Sambamba na hayo amesema faida mbalimbali amepata wakati
alipokuwa kiongozi wa skuli hiyo ikiwemo kujiona mzalendo,kuongeza
ujuzi,kujiamini katika sehemu yoyote .
Mwanafunzi wa Skuli hiyo Hunaida Haji Juma alisema kuna
tofauti mbalimbali za kuongoza kwa mwanaume na mwanamke.
" Mwanamke anazidi kukemea suala la udhalilishaji
tofauti na mwanaume,vilevile mwanamke anatoa nafasi za uwongozi mbalimbali kwa wanawake wenzake tofauti na
mwanaume .
Sambamba na hayo amesema kuna idadi ndogo ya viongozi
wanawake maskulini hasa katika nafasi za uraisi.
" Takribani ya skuli nyingi maraisi wanaume baadhi ya
skuli ndio utakuta raisi mwanamke ikiwemo skuli ya faraja, bembela na alhisani
na skuli hizi mbili kwakuwa hawana wanaume ndio ilapelekea wanawake kuwa
raisi." alisema hunaida
Mwanafunzi wa Skuli
ya Lumumba Imraan Iddi Hamadi alisema nafasi za uwongozi ni chache kuanzia
ngazi za skuli hadi katika tasisi nyengine kutokana na kuwepo kwa mfumo
dume,usawa wa kijinsia,pamoja na wanawake kutokuwa na muamko wa kuweza
kuongoza.
" Kuna sababu nyingi ambazo zinawafanya wanawake kuwa
nyuma katika nafasi za uwongozi ikiwemo kutokuwepo kwa usawa wa kijinsia
kwasababu nafasi nyingi wanapewa wanaume za uwongozi kuliko wanawake nahii
inatokana na kuona kuwa wanawake hawawezi kuongea au kujituma." alisema
Mwanafunzi wa Skuli ya
Lumumba Salima Shamimu khamis
amesema kuna faida mbalimbali ambazo zinapatikana endapo mwanamke akiwa
kiongozi ikiwemo kutakuwepo na usawa wa kijinsia,mwanamke kuchanganua vitu
mbalimbali pamoja na kufanya ubunifu kwa lengo la kuinua uchumi wa nchi.
Pia amewaaasa
wanafunzi wenziwe kuchangamkia fursa katika nafasi mbalimbali za uwongozi
katika skuli itamsaidia kupiga hatua hadi kufikia nafasi za juu za uwongozi.
Mwalimu wa Skuli ya
Sekondari Bembela Abdallah kombo khamisi
amethibitisha kuwa kuna sababu nyingi ambazo zinawanyima nafasi za uwongozi
wanawake .
" Wanaume wengi wamepata taaluma ya uwongozi kuliko
wanawake,wanaume wanajiamini mbele za
watu kuliko wanawake ,pamoja na baadhi ya watu kuwa na itikadi za kidini kuwa
mwanamke hawezi kuwa kiongozi." alisema
Pia amesema licha ya kuwepo kwa mitazamo hiyo kwa watu
lakini wanawake wameeanza kuchangamikia fursa hiyo kwa kupata taaaluma za
uwongozi kuanzia nganzi ya nchini hasa mashuleni hadi nafasi za juu.
Aidha amesema ili kuwepo kwa idadi nyingi ya viongozi
wanamke inahitajika kupewa elimu katika sehemu mbalimbali ikiwemo mashuleni
hadi katika shughuli mbalimbali za kijamii.
" kila mtu anahaki ya kuongoza na ili mwanamke aweze
kupata nafasi katika uwongozi waanze kupewa elimu tangu wakiwa skuli za msingi
kwa lengo la kumjenga na kweza kujiamini hii itamsaidia kwa kupenda kuongoza hadi kufikia nafasi za juu
bila ya uwoga.
0 Comments