Ticker

6/recent/ticker-posts

Kiwango Kikubwa Cha Fedha Kuwakwamisha Wanawake Kugombea Uongoazi.

 


NA ASIA MWALIM:

WANAWAKE wanaotaka kugombea nafasi za uongozi Zanzibar wameiomba serikali kupunguza gharama ya fomu hizo ili iwe rahisi kwao kushiriki katika haki yao ya msingi na kidemokrasia.

Walisema hayo wakati wakizungumza na muandishi wa habari hizi kwenye maeneo mbali mbali ya Zanzibar.

Nadhira Ali Haji, (50) Mwanachama wa Chama Cha CUF, alisema uchaguzi wa mwaka 2022 alikua ni mwanamke wa kwanza kutangaza nia yake ya kugombea nafasi ya urais Zanzibar lakini ilishindikana.

"Miongoni mwa changamoto inayojitokeza kwa wanawake wanapotaka nafasi za uongozi ni kushindwa na rasilimali fedha za kuchukulia fomu hizo" alisema.

Alisema nia yake ya kugombea nafasi ya urais kupitia chama cha CUF, imekuja kutokana na uwezo wake wa kujiamini, na uwajibikaji kwa moyo thabiti na wala hakushawishiwa na mtu.

Alieleza kuwa baada ya kamati ndani ya Chama chake kuridhia kuwa mwanamke huyo atagombea nafasi ya urais ambayo ndio ngazi ya juu kabisa hapa nchini, alipata faraja kwa kuwa ana uwezo wa kutumika nafasi yoyote.

Bahati Khamis na Khadija Miraji wanawake kutoka Chama Cha CUF, walisema walifurahishwa na hatua aliochukua mwanamke huyo na hawakuwa na shaka kumpatia nafsi hiyo kwa kua na kila kigezo cha kuongoza.

"Tumemuona anafaa ndio manaa tuka mchagua na kamati iliamua kumpitisha ili kuingia katika kinyanganyiro hicho lakini hakufanikiwa baada ya kukosa fedha za kuchukulia fomu" walisema

Walieleza kusikitishwa na jambo hilo ambalo lilikosa msaada na utatuzi ndani ya chama chao, hivyo kupelekea bi nadhira kushindwa kugombea uongozi.

Mkurugenzi wa Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar, Jamila Mahmoud amevitaka vyama vya siasa kumuunga mkono Wanawake kwa kuwawezesha kifedha sambamba na kuketa msukumo kwa wanawake kujitokeza kwa wingi kuwa viongozi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania -Zanzibar (TAMWA) Dk. Mzuri Issa, alisema wanawake wanakumbana na changamoto nyingi katika kutafuta nafasi za uongozi, jambo ambalo linarudisha nyuma jitihada zao.

Alisema wameshatoa mafunzo mara kadhaa kwa waandishi wa habari na wameonesha utayari wao wa kushiriki uongozi ingawa kuna vikwazo vyengine ikiweko suala la fedha kwa wanawake wanaotaka kuchukua fomu za kugombea nafasi hizo.

Katika uchaguzi wa mwaka 2020 baadhi ya vyama vya siasa vilitoa fomu za kugombea uongozi kwa shilingi milioni moja kwa nafasi ya Urais, shilingi laki mbili kwa nafasi ya uwakilishi na shilingi elfu 50 kwa nafasi ya udiwani.

Post a Comment

0 Comments