Na Ahmed Abdulla, Zanzibar:
Hii
ni karne ya 21ambayo Kasi ya technolijia inazidi kuimarika duniani.
Zanzibar
nayo ni sehemu ya dunia ambayo matumizi ya teknolojia hiyo yamekuwa kwa kasi.
Mitandao
ya kijamii ni sehemu ya teknolojia hiyo ambayo kwa Takwimu kutoka Mamlaka ya mawasiliano
Tanzania (TCRA) hadi kufikia mwezi Disemba 2023 watanzania 34,469,022 kati ya 61,741,120
wa wanatumia huduma za intaneti hiyo ikiwa na maana wanatumia mitandao ya
kijamii.
Zanzibar
ikiwa ni miongoni mwa nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
watu wake hawako nyuma katika matumizi ya mitandao ya kijamii lakini jee
wanawake wanaitumia mitandao hiyo kwenye kusaka uongozi?
Suhaila
Ussi Pondeza ni mjumbe wa kamati ya utekelezaji Umoja wa wanawake wa chama cha
Mapinduzi Tanzania (UWT) wilaya ya Amani Kichama alisema licha ya kuwa na Kurasa
za mitandao ya kijamii lakini hatumii kwenye harakati zake za kisiasa.
“Sasa
naanza kushawishika kwenye kutumia mitandao ya kijamii kwenye harakati zangu za
kisiasa maana naweza kuwafikia watu wengi kwa muda mfupi” alisema Suhaila
Maua
Mohammed Mussa ni mwanasiasa mwanamke ambaye Mwaka 2020 aligombea nafasi ya
Ubunge jimbo la Shaurimoyo kwa tiketi ya Chama Cha ACT-Wazalendo alisema
hakutumia mitandao ya kijamii kwenye harakati zake za kuwania nafasi hiyo huku
akiitaje elimu ya matumizi ya mitandao hiyo ndio ilikuwa changamoto kwake.
“Nafahamu
kwamba nilikosa mengi kwa kukosa kwangu kutumia mitandao ya kijamii likini
tatizo kubwa ni kuwa wanawake wengi tuna changamoto ya kutokuwa na elimu juu ya
matumizi ya mitandao hiyo” Alisema
Kwa
upande wa katibu wa Umoja wa Wanawake Wa Chama cha Mapinduzi Tanzania (UWT) wilaya
ya Kati alisema wanatambua kuwa wanasiasa wanawake wa chama hicho bado hawana
muamko wa kutumia mitandao ya kijamii kwenye masuala ya siasa ilhali ndio
sehemu yenye kundi la watu wengi.
“Tunachokifanya
kwa sasa ni kuwashawishi wanawake watumie mitandao ya kijamii kwani kuna fursa
kubwa ya kujitangaza” Alisema
Mkuu
wa kitengo cha habari na mawasiliano kutoka chama Cha Waandishi wa Habari
Wanawake Upande wa Zanzibar (TAMWA-Zanzibar)Sofia Ngalapi alisema TAMWA
imebaini kuwa wanasisa wengi wanawake wanazo kurasa za mitandao ya Kijamii
lakini wanashindwa kuitumia fursa iliyopo huko kwa ajili ya kufanikisha malengo
yao.
“Wengi
wao wanazo kurasa za mitandao ya kijamii lakini hawazitumii kwenye harakati zao
za siasa ila wajuwe wanakosa fursa ya kujitangaza kwa watu wengi ndani ya muda
mfupi” Alisema
Pia
aliwasisitiza wanasiasa wanawake na vijana kuitumia mitandao ya kijamii katika
kubadilishana mawazo na wanasiasa wabobezi wanaotumia mitandao hiyo.
Kwa
muktadha huo inaonyesha kuwa Licha ya fursa nyingi zilizopo kwenye mitandao ya
kijamii lakini bado wanasiasa wanawake wako
kwenye usingizi mzito juu ya matumizi ya mitandao hiyo.
Ni
jambo jema sasa kwa kila mwanasiasa mwanamke kuanza kutumia mitandao ya kijamii
kwenye harakati za siasa ili kuona wanafika kule ambako wanaharakati wa
kupigania usawa wa kijinsia kwenye uongozi na demokrasia hasa kwa kuzingatia ni
mwaka mmoja tu umesalia kabla ya kufika kwa uchaguzi mkuu wa dola visiwani
Zanzibar.
0 Comments