Na Thuwaiba Habibu:
Mwenyekiti
wa kamati ya utetezi kutoka Chama Cha Waandishi Wa Habari TAMWA Bi Shifaa Said Hassani amewapongeza waandishi
wa habari chipukizi kwa kuutendea haki
mradi wa wanawake na uongozi kwa kufanya kazi kwa kitaalamu zaidi.
Ameyasema
hayo katika sherehe ya mahafali ya waandishi
wa habari chipukizi yaliofanyika
ukumbi wa bima Zanzibar alisema
waandishi wa habari chipukizi wameweza
kutendea haki mradi wa wanawake na uongozi pamoja na kuweza kuibua vitu mbalimbali ikiwemo
changamoto za wajasiriamali wa Micheweni.
Pia alisema
wameandika habari pamoja na makala zenye taaluma na ubunifu kwa kuangalia
mikataba ya kikanda na kimataifa.
"tumezowe kuona makala zinazomuhusu mtu
anahojiwa mtu mmoja peke yake lakini wao walitumia vyanzo tofauti tofauti vya
habari na kazi zao ambazo amefanywa
ziliandikwa kitaalamu kwani wengine kusubutu kutumia mikataba ya kikanda na
kimataifa."
Pia
aliwataka waandishi hao wasifanye mahojiano marefu ili kuleta ladha zaidi
katika makala zao.
Alisema
changamoto ambayo niliona ndani ya makala mulizofanya ni mohojiano marefu suala ambalo nimenifanya
nijilazimishe kusikiliza na kusoma.
Aidha
alisema kwa mwaka huu kidogo waandishi wamelisahau kundi la watu wenye ulemavu
na kuwataka waandishi wajisongeze karibu na watu hawa kwani hizi ni sauti za
wasio sauti
"Hata kama hatukuwaweka katika makala
zetu basi japo tuwafanyie mahojiano na wao wawe miongoni mwa walioshiriki
alieleza."
Nae mjumbe wa bodi ya Tamwa bi Hawra shamte
aliwaomba waandishi hao waweze kuwa
ngangari na kutekeleza vigezo vyote vya uandishi wa habari kwa kutumia kalamu
zao Vizio ili kuhakikisha sauti za wanawake, vijana,watoto na watu wenye
ulemavu zinasikika.
Alisema
munatakiwa kuwa waadilifu na kufuata maelekezo ya uandishi wa habari na
tusifanye kazi kwa kutegemea kitu na
tufanye kazi kwa ajili ya kutetea jamii yetu.
Hata hivyo
aliwashukuru wahariri na wasimamizi kuwasimamia kufanya utendaji kazi ulio
imara.
"
Mumeonesha kujitoa na kutuheshimisha kwa kuhakikisha wanawake wanapata nafasi wanazo stahiki na naamini kuwa nyinyi ndio
wahariri wa baadae".
Nao wahitimu
wa mradi huo Berema Suleman Nassor na Nihifadhi Abdallah Issa walitowa
shukurani kwa chama cha waandishi wa habari wanawake Tamwa kwa kuweza kuwapatia
mafunzo yaliyoweza kuwafunza namna ya
kuandika habari za wanawake na uongozi
Awali
walikuwa hawajuwa kitu gani wafanye katika kukamilisha kazi hii lakini kutokana
na mafunzo waliopatiwa waliweza kujuwa kuandika hata kwa kutumia mikataba mbali
mbali
Vile vile walisema kuna changamoto mbali mbali walizokabiliana na lakini walihakikisha wanazishinda ili kukamiliza kazi hizo.
0 Comments