Mbunge Wa wananchi wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza amekutana na wanafunzi wanawake
Wa Madrasa mbalimbali za jimbo la Chumbuni kwa lengo la kutatua
Changamoto zao Zikiwemo Vikalio, Mafeni, Ukarabati Wa Nadrasa.
Katika mazungumzo yao Pondeza alisema yale yote yaliyo
katika uwezo wake atayafanikisha ili utoaji na upatikanaji wa elimu uwe katika
mazingira bora.
“Nitahakikisha nafanikisha yale yote yaliyo katika uwezo
wangu kwa haraka” Alisema
Aidha mbunge huyo aliwasisitiza wanafunzi hao kusoma kwa
bidii ili kuona jimbo hilo linakuwa ba wataalamu wengi wa masomo ya dini ya
kiislamu.
“Jimbo hili linategemea uwepo wa wataalamu wa masomo ya dini
ya Kiuslamu hivyo someni kwa bidii kufikia lengo hilo” Aliongezea
Wanafunzi hao walimuahidi mbunge huyo kusoma kwa bidii ili
kufanikisha lengo la kuwepo kwa wataalamu hao.
0 Comments