Na Ahmed Abdulla, Zanzibar:
Wanawake wenye ulemavu wanamchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya
taifa na nafasi katika kukuza demokrasia
nchini.
Maendeleo hayo si kwamba yatamfaa Mwenye ulemavu pekee bali hata
asiyekuwa na Ulemavu.
Katika uchaguzi wa mwaka 2020 Zanzibar iliandikisha wapiga kura
566,352 lakini waliopiga kura ni watu 498,786.
Katika watu hao waliopiga kura watu wenye ulemavu walikuwa ni 4680
ambao wanawake kati yao ni 2197 na wanaume ni 2483.
Lakini kwa upande wa wagombea wanawake wenye ulemavu kwa nafasi
mbalimbali kuanzia wadi hadi Taifa kulikuwa na wagombea mgombea mmoja tu na
ilikuwa ni nafasi ya Udiwani.
Hii inatokana na vyama vya siasa kutokuwa na utamaduni wa kuibua
vipaji vya viongozi wanawake wenye ulemavu kwani hata hao wachache walioomba
ridhaa ya kugombea sehemu Fulani hawakuteuliwa na vyama vyao.
Tunu Juma Kondo ni Naibu Katibu Mkuu Umoja wa wanawake Tanzani upande
wa Zanzibar, Chama Cha Mapinduzi (UWT) amesema bado wanawake wenye Ulemavu
wamemekuwa waoge kwenye kugombania wadi, majimbo na Uraisi.
“Tumeweka nafasi maalum za watu wenye ulemavu kwenye uwakilishi na
ubunge kwani tunaona bado wana uoga wa kenda majimboni na kwenye wadi”
Bi. Tunu pia amewasisitiza wanawake wenye ulemavu kuondoa hofu pale
wanapohitaji kugombea sehemu yeyeote.
Jamila Borafia Hamza ni mwanamke wenye ulemavu wa uoni, aliwahi
kugombea nafasi ya uwakilishi katika jimbo la Mwanakwerekwe kuptia Chama Cha
Mapinduzi, hakufanikiwa kinyanganyiro hicho aliishia chaguzi za ndani ya jimbo.
Alisema moja ya changamoto aliyokutana nayo ni kukosa usafiri wa
uhakika kuwafuata wajumbe kwa ajili ya kunadi sera zake.
“kama Tunavyotambua wajumbe hawaka katika eneo moja na mtu mwenye
ulemavu hawezi kwenda peke yake, kwa hiyo kumfuata mjumbe mmoja baada ya
mwengine ni kipengele na wengi wetu tunashindwa hapo” Alisema Jamila
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Chama Cha Ada Tadea Juma Ali Khatib
alisema chama chao kinawapa nafasi kubwa wanawake wenye ulemavu wanapojitokeza
kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
“tulikuwa naye mgombea mmoja mwanamke mwenye ulemavu na aligombea
ubunge wa Kikwajuni, tulimsaidia mambo mbalimbali hata kumbeba kumuweka kwenye
jukwaa ili aombe kura” Alisema Juma Ali Khatib
Kauli ya serikali ni ipi juu ya wanawake wenye
uongozi wenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi?
Katibu Mtendaji wa baraza la watu wenye ulemavu, ofisi ya makamu wa
kwanza wa Raisi Zanzibar Ussi Khamis Debe alisema ofisi inatajia kukutana na
vyama vya siasa kwa lengo la kuwawekea mazingira wezeshi wanawake wenye ulemavu
ili wafanikishe azma zao bila uwepo wa changamoto zinazosababishwa na ulemavu
wao.
“kubwa linalokuja ni kuweka mazingira wezeshi ya Kampeni, kwamba
majukwaa yaendene na hali za watu wenye ulemavu husika” alisisitiza
Ni dhahiri kuwa bado wanawake wenye ulemavu hawajawa na muamko mkubwa
kwenye kugombea nafasi za uogozi katika wadi, majimbo na hata uraisi.
Hivyo ni budi kwao kujitokeza kwa wingi kwenye vinyanganyiro vya
nafasi hizo na vyama vya siasa viwaunge mkono kwa asilimia mia kwenye mchakato
wao wa uchaguzi
0 Comments