Na Ahmed Abdulla:
WAANDISHI wa Habari nchini
wametakiwa kuandika habari zinazohusu Wanawake kuzingatia vigezo vya kiuandishi
ili kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi
wa chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania Upande wa Zanzibar TAMWA-ZNZ
katika hafla maalum ya utoaji wa Tunzo za umahiri wa Uwaandishi wa habari za
Takwimu iliyofanyika ukumbi wa Shaa Mjini Unguja.
Alisema endapo waandishi wa
habari watajikita kwenye kuandika habari za matokeo chanya yanayofanywa na
wanawake basi lengo la kufikia asilimia 50 kwa 50 kwenye nafasi za uongozi
nchini litafikiwa.
“Tunaamini wanawake wanaweza
kuwa active zaidi katika masuala ya uongozi endapo waandishi wa habari
wataandika habari kuhusu wao” Alisema Dkt. Mzuri Issa
Mtakwimu mkuu wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar Salum Kassim Ali yeye aligusia suala la vitendo vya ukatili wa
wanawake na watoto na kueleza kuwa, Takwimu zinaonesha kuongezeka kwa idadi ya
vitendo vya udhalilishaji hivyo waandishi wa habari wanawajibu mkubwa kuendelea
kuandika habari ili kuchangia mabadiliko chanya katika jamii juu ya vitendo
hivyo.
“Takwimu kutoka ofisi ya
Mtakwimu Mkuu wa Serikali zinaoesha kuwa, mwaka 2020 jumla ya matukio 1360
yameripotiwa, 2021 matukio 1361, 2022 matukio 1366 huku mwaka 2023 matukio 1994
yameripotiwa ya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia,” ameelezaa.
Aliongeza kuwa kwa mwezi wa Januari 2024 jumla ya matukio 1760 ya
wanawake kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia
yameripotiwa Zanzibar.
“Kiukweli idadi ni kubwa sana
ya matendo haya ya udhalilishaji hivyo niwaombe ndugu zangu wanahabri kuongeza
jitihada katika kuandika ili kuweza kupunguza haya matendo ambayo yanatia doa
Zanzibar,” ameeleza.
Mapema Afisa kutoka Mamlaka ya
kuia na Kupambana na Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) Yusuf Juma
Suleiman ameahid mashirikiano baina ya ZAECA na Waandishi wa habari katika
kutekeleza majukumu yao kila siku.
“Waandishi sis ZAECA tunaahidi
mashirikiano na nyinyi kattika kutekeleza majukumu yenu hususani kuandika
habari rushwa ya ngono ambayo nayo imekithiri,”ameeleza.
Jumla ya kazi 525 ziliwasiliswa
kwa ajili ya kuwania tuzo hizo ambapo kwa upande wa waandishi wa Magazeti tuzo
ilikwenda kwa Asya Mwalimu wa gazeti la Zanzibar Leo, waandishi wa Radio za
kitaifa tuzo ilikwenda kwa Huwaida Nassor wa Radio Assalaam Fm, waandishi wa
Radio za kijamii tuzo ilikwenda kwa Amina Massoud Jabir kutoka Radio Jamii
Mkoani na Waandishi wa mitandao ya Kijamii tuzo ilikwenda kwa Zuhura Juma Said huku msindi wa jumla akiwa ni
Amina Massoud Jabir wa Radio Jamii Mkoani.
0 Comments