Katibu Mkuu
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Abeida Rashid Abdallah
amewataka Watoto wakike wenye ulemavu kutoona hali hiyo kwamba ni kikwazo cha
kutosoma na kukatisha ndoto zao za Maisha.
Akizungumza
na wasichana hao katika uzinduzi wa vyoo rafiki kwa Watoto wa kike wenye
ulemavu uliyofanyika katika skuli ya Sekondari ya Jangwani Dar Es Salaam, hafla
hiyo imeandaliwa na Taasisi ya Maisha ya Amani kwa watu wenye ulemavu, amesema
anaelewa changamoto zinazowakabili wasichana hao lakini hawatakiwi kukataa
tamaa katika kutafuta elimu ili wawe viongozi wa baadae.
Amesema
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
zinazungumza masuala ya watu wenye ulemavu kwenye vyombo vya maamuzi ili
kuhakikisha watu wenye ulemavu hawajaachwa nyuma.
Amesema nchi
ya Tanzania inamingozo mbali mbali ambayo inasimamia masuala ya watu wenye
ulemavu ikiwemo UN Covection on the right of People with disability pia
kunasheria ya Tanzania Bara ya 2010 kwa
upande wa Zanzibar kuna sheria namba 9
ya mwaka 2006 ambayo imefanyiwa marekebisho mwaka jana, sheria zote hizo
zinazungumzia wajibu wa utambuzi wa haki kwa watu wenye ulemavu, usawa na
kutokubaguliwa, kukuza uelewa, n.k.
Aidha Katibu
Mkuu huyo ametoa wito kwa walimu wote katika skuli mbali mbali kuweka vyoo
rafiki kwa Watoto wenye ulemavu, na sio vyoo tuu hata njia ili mazingira nayo
yawe rafiki ili wajihisi wako na amani.
Naye
Mkurugezi wa Taasisi ya Maisha ya Amani
kwa watu wenye ulemavu, Sofia Mbeyela amesema mradi huyo wa ujenzi wa vyoo
rafiki kwa Watoto wa kike wenye ulemavu umeanza Julai mwaka jana na umegharibu
milioni 20,000 kwa kujenga vyoo vine na chumba kimoja kwaajili ya wasichana hao
kubadili nguo wakati wakiwa katika siku zao za hedhi.
Aidha
amewashukuru wadau wote waliyojitokeza kwa hali na mali katika kuchangia ujenzi
huo kwani hapo awali skuli hiyo ilikuwa
na vyoo rafiki vitatu huku wanafunzi wakiwa 110.
Amesema
mradi huo utaendelea kwa skuli zote hivyo amewaomba wananchi, viongozi,
mashirika/taasisi za umma na Serikali kuendelea kuchangia mradi huo ili
kuwaondolea Watoto wenye ulemavu changamoto hiyo.
Kwa upande
wa wanafunzi wenye ulemavu, akizungumza Zulfa Swaleh mwanafunzi wa kidato cha
kwanza katika Skuli ya Jangwani amesema amefarajika na ujenzi wa vyoo lakini
pia amewaomba wananchi kujitokeza kuwasaidia madaftari na vitavu kwani wengi
wao ni Watoto wa familia za kipato cha chini.
Mkurugezi wa Taasisi ya Maisha ya Amani kwa watu wenye
ulemavu, Sofia Mbeyela na Katibu Mkuu
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Abeida Rashid Abdallah ni
watu mweney ulemavu hivyo wanaelewa changamoto zinazowakabili Watoto wenye
ulemavu na wataendelea kupambana ili kuhakikisha watu wenye ulemavu hawajaachwa
nyuma.
0 Comments