Ticker

6/recent/ticker-posts

Maoni Ya Marekebisho Sheria Ya Mtoto Yaendelea Kupokelewa



Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Siti Abass Ali amesema Idara hiyo ipo katika mchakato wa kukusanya maoni kutoka kwa wadau mbali kwaajili ya kuifanyia maboresho sheria ya Mtoto namba sita (6) ya mwaka 2011 ili iendane na wakati uliyopo.


Akizungumza katika kikao cha ukusanyaji wa maoni kilichowashirikisha  wadau mbali mbali wakiwemo viongozi wa dini, wanasheria, Jeshi la Polisi, n.k  katika ukumbi wa Skuli ya Kidonge Chekundu Unguja, jana alisema kutokana na vitendo vinavyojitokeza katika jamii,ikiwemo ajira za utotoni hivyo, idara hiyo imelazimika kuipitia sheria hiyo nakuja na maamuzi ya kuifanyia maboresha ili iendane na wakati .

“Kwa kweli Sheria hiyo  imetusaidia sana na inaenaendelea kutusaidia, imezungumza umuhimu wa mtoto kupata haki zake za msingi ikiwemo haki ya kupata elimu, matibabu, chakula, malazi, malezi, pia imezungumzia jinsi gani mtoto ataepukana na masauali ya udhalilishaji lakini baada ya kuipitia sheria hiyo tumeona bora tuifanyie maboreshao ili iwe nzuri zaidi, pia tumeona  ni ya muda kidogo, tangu ilipotungwa hadi leo ni miaka kumi na mbili na  vitendo vinaendelea kujitokeza kama hili suali la ajira za utotoni ni changamoto kubwa” Alisema Siti.

Alisema katika ukusanyajji wa maoni wameanza na makundi ya watoto kupitia mabaraza ya watoto, viongozi wa dini, waandishi wa Habari, waratibu wa kupinga vitendo vya ukatili na udhalilishaji, Wizara na Taasisi mbali mbali za Umma na Binafsi, wakiwemo Wizara ya elimu, Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka (DPP), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Zanzibar (TAMWA-ZNZ), Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA), n.k.

Aidha Mkurugenzi Siti alifafanua kwamba umuhimu wa marekebisho ya Sheria ya  mtoto ni pamoja na maendeleo ya sayansi na teknolojia  ambayo kimsingi yameongeza haja ya kuimarisha baadhi ya vipengele katika sheria hiyo.



Naye Mkuu wa Divisheni ya Watoto wa Idara hiyo Mohammed Jabir alisema kipengele namba 18 cha uanzishaji na uendeshaji wa mahakama ya Watoto kimeeka wazi aina ya makosa na muda ambao mshatakiwa atapaswa kutumikia adhabu au kifungo lakini adhabu hiyo sio kali hivyo ni wazi kwamba marekebisho  yanahitajika katika kupengele hicho.

Pia alisema kipengeleza namba 12 kimezingatia majukumu ya wazazi katika kuwasiamia Watoto ila bado wazazi hawakielewa na kukitumia kinavyotakiwa katika kuleta mageuzi ya malezi bora kwa Watoto, hivyo kanuni inahitajika ili iweze kutoa miongozo.

Kwa upande wa washiriki wa mkutano ambao ni wadau wa kupinga Vitendo vya Ukatili na Udhalilishaji wa kijinsia wamesema Sheria ya Mtoto namba 6 ya mwaka 2011 ni vyema ikatambua mgawanyo  wa haki za watoto kwa kuzingatia umri ili kulinda maslahi na ustawi wa mtoto.


Akizungumza  Hakimu dhamana Mkoa wa Kusini Unguja  Khamis Rashid Khamis  amesema ni wakati sahihi  wa kueka sheria ambayo Itatoa muongozo wa kushughulikia watoto wenye umri wa chini ya miaka 14  na 16 na kuweka utaratibu wa kusikiliza kesi zao.


Idara ya Maeleleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inaendelea na ukusanyaji wa maoni kwa kukutana na makundi mbali mbali katika jamii  kwa lengo la kuipata maomi ili sheria mpya iwe   nzuri kwa na yenye maslah kwa mtoto.




Post a Comment

0 Comments