Na Ahmed Abdulla, Zanzibar
Jamii na baadhi ya familia zimeaminishwa kama mwanamke siku zote hawezi kuwa kiongozi, ikiwa ndani ya familia au nje ya familia kwa visingizio tofauti vinavyoaminika na baadhi ya jamii hizo.
Kwa karne kadhaa ama miongo iliyopita akili za walio wengi
zilipikwa na kuaminishwa dhana hiyo potofu amabayo siyo sahihi kama walio wengi
wanavyoipokea na kuifanyia kazi.
Mwanamke ni kiumbe aliepewa akili kama mwanamme, busara,hekima
na hata uwezo wa kufikiri na kutoa maamuzi yanayofaa.
Na kwa bahati nzuri mfano hai unaonekana katika nchi ya
Tanzania, kiongozi mwenye nafasi ya juu anaeongooza watanzania ni mwanamke, nae
ni mama Samia Suluhu Hassan ambae ni Rais wa Jamhuri wa Tanzania.
Na kama hiyo haitoshi Zanzibar mwana mama Zena Ahmed Said ndie
katibu Mkuu Kiongozi wa Baraza la Mapinduzi, amabae ni mwanamke wa mwanzo
kushika wadhifa huu tokea kufanyika kwa Mapinduzi ya Zanzibar
yaliyoung’owa utawala wa Sultan katika
utawala wake na Zanzibar kujitawala wenyewe.
Kwa mujibu wa kauli ya Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi amedhihirisha wazi katika moja ya hutuna
zake kwa kusema katika Mawaziri aliyowateuwa ndani Serikali ya M apinduzi
Zanzibar wanawake wanafanya vizuri.
“Katika Mawaziri niliwateuwa basi wanawake hawajawahi
kuniangusha,” Rais Dk Mwinyi.
Pamoja na hayo Zanzibar ni nchi kama nchi nyengine duniani
ambayo imeridhia mikataba mbali mbali inayotetea usawa wa kijinsia katika mambo
mbli mbali yanayowahusu.
Mikataba
hiyo ni pamoja na Tamko la Kimataifa la haki za binadamu (Universal Diclaration) na mkataba wa Haki za Kiraia na Kisiasa (ICCR) ambayo Tanzania ni
moja ya nchi iliyoridhia mikataba hiyo, ambapo nchi mia moja na sabiini na mbili
(172) zimeridhia mkataba wa haki za kiraia na kisiasa.
Mkataba mwengine ni mkataba wa Bara la Afrika unaojuilikana kama mkataba wa
haki za binadamu na haki za watu wa Umoja wa Afrika, uliopitishwa mwaka 1981
(Afrika Charter on Human Peoples Right)
ulianza kutumika (1986) na mkataba huo
hadi kufikia mwaka (2002) tayari ulisainiwa na nchi mia moja hamsini na tatu
(153) za Afrika.
Hata hivyo dini ya kiislam ina nafasi yake katika
nafasi ya mwanamke na Uongozi, mmoja kati ya wahadhiri wa kiislam visiwani Zanzibar
Ukhti Amina Salim amesema kila mmoja katika jamii inapaswa kushirikishwa katika
hadhi yake na nafasi yake kwa sababu maisha ni ya watu wote baina ya mwanamke
na mwanamme.
“Kwa mda mrefu wanawake wamekosa kushirikishwa
katika vyombo vya maamuzi na hali hii inasababisha uharibifu na kutokuwa na
maendeleo katika jamii hiyo,” Ukhti Amina.
Maryam Ame
Choum ni mratibu wa mradi wa kuinuwa wanawake katika harakati za Uongozi kutoka TAMWA,ZANZIBAR amesema wametowa
mafunzo kwa wanawake wapatao themanini kwa Unguja na Pemba kutoka katika vyama
vya siasa na wanafunzi kutoka vyuo vikuu , ambapo kupitia mafunzo hayo wanatarajia wanawake wengi Zanzibar
watajitokeza kugombea nafasi za Uongozi katika Uchaguzi mkuu wa October 2025.
Zawadi Hamdu Vuai ni Diwani wa Wadi ya Kiungoni
Makunduchi amesema anaongooza nafasi hiyo kwa takribani miongo mitatu kupitia
wadi tofauti, alianza kuhudumu nafasi ya Uongozi tokea mwaka 2008 akiwa mratibu
wa wanawake na watoto na mwaka 2010 alichaguliwa kuwa mwanamke wa kwanza kutoka
vijijini kuchaguliwa kupata mafunzo ya Uongozi kupitia Chama cha Waandishi
wahabari wanawake Tanzania Zanzibar TAMWA ZNZ.
“Chanagamoto za Uongozi ni nyingi lakini sikukata
tamaa nilipambana nazo kuhakikisha nafikia malengo yangu katika jamii na Zaidi
ni uthubutu na kujiamini ndio siri ya mafanikio,” Zawadi Hamdu.
Nae Satia Mussa kutoka chama cha Sauti ya Umma (SAU)
amesema ana nia ya kugombea nafasi ya Uongozi kwa sababu ameshapata mafunzo ya
Uongozi kupitia TAMWA na yamemuwezesha kumjengea uthubutu na ujasiri.
“Katika kugombea lazima ushirikishe familia na jamii
husika ili kufanikisha malengo yako, walezi wa familia ni wanawake ila walio
wengi walikuwa hawajitambuwa,” Satia Mussa.
Ndoto ya kufikiwa 50% kwa 50% katika nafasi za
Uongozi itafanikiwa iwapo wanawake wenye uwezo wa kuongoza nafasi mbali mbali
za Uongozi watapewa nafasi kuanzia ngazi ya familia,kitongoji, shehia, Taasisi
na kushika nyadhifa katika Serikali kuu.
0 Comments