Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Riziki Pembe Juma amewataka wananchi kuzingatia umuhimu wa Afya ya
akili ili kuzuia maafa ambayo yanayoweza kutokea na kupelekea athari kubwa kwa
katika mwili wa binadamu.
Akizungumza katika bonanza la kuadhimisha kuelekea siku ya afya
ya akili na maafa duniani lilofanyika katika jengo la Chuo cha Afya Zanzibar
Wilaya ya Magharib “B” Unguja, amesema
kila mwananchi anapaswa kutambua umuhimu wa afya ya akili kama ilivyo
afya ya mwili ili kujikinga na maafaa ambayo yanawezakujitokeza.
Amesema afya ya akili ni muhimu kwa kila mtu
kwani inamuwezesha kuishi maisha yenye furaha, tija na kujisikia vizuri
ulimwenguni. Lakini mara nyingi suala hili halipewi kipaumbele kinachostahili. Hivyo Waziri huyo amehimiza suala la afya ya akili kupewa
kipaumbele na kila mtu, kutambua kwamba
ni sehemu muhimu ya afya kwa ujumla.
“Afya ya Akili ni muhimu kwa kila mmoja wetu,
kwani maafa hayachagui mtu wa
kumuathiri, yanaweza kumuathiri mtu yeyote, mahali popote, wakati wowote”
Alisema Waziri Pembe.
Alifahamisha kwamba kila ifikapo tarehe 13
Oktoba, huadhimishwa Siku ya Afya ya akili na maafa Duniani, siku hii
inawakumbusha watu/jamii juu ya umuhimu wa kuwa tayari katika kukabiliana na
maafa yanayoweza kutokea. Pia alisema
siku hiyo huongeza uelewa wa afya ya
akili na kuleta mabadiliko chanya kwa afya ya akili ya kila mtu.
Aidha Waziri Pembe alisema mwaka huu 2023,
katika kuadhimisha Kimataifa siku ya Afya ya akili itachunguza uhusiano wa pande
mbili kati ya maafa na usawa wa kijinsia, hivyo amewaomba wananchi kupenda kukuhimizana kushiriki katika kila tukio la
kuendeleza umoja, au kujiunga na mazungumzo juu ya kupambana na usawa wa
kijinsia kwa ajili ya maendeleo ya nchi
yetu.
Mapema Mkurugenzi Mtendaji Chuo cha Afya
Zanzibar (ZSH) Aziza Hemed ametoa wito kwa wananchi kuwa mabalozi wazuri
kuhamisha jamii kupata ushauri nasihi na kisaikolojia pale ambapo wanapopata
matatizo za kimaisha kwani hatua hiyo inaweza kupunguza athari za maafa ambazo
zinatokana na binadamu.
Kupitia bonanza hilo shughuli mbali mbali
zimeandaliwa ikiwemo debeti,michezo,utowaji wa zawadi pamoja na zoezi la
kuhitimisha program ya mafunzo ya msingi “Crash Program”.
0 Comments