Na Ahmed Abdulla:
Wizara ya Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inaendelea kuratibu Pencheni jamii kwa
kushirikiana na taasisi mbali mbali wakiwemo Wizara ya Nchi (OR) Fedha na
mipango na kusimamia wazee wasio na vyeti vya kuzaliwa ili kuhakikisha na
wanapata vyeti hivyo na jambo litakalowasaidia kupata fursa mbalimbali.
Hayo yalielezwa na
waziri wa wizara hiyo Riziki Pembe Juma huko ofisini kwake Kinazini, Zanzibar
wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu siku ya wazee duniani
itakayoadhimishwa Oktoba 01, katika ukumbi wa Dkt. Ali Mohammed Sheni – SUZA
ambapo Mgeni ramsi anatarajiwa kuwa Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza
la mapinduzi Dkt. Hussei Ali Mwinyi.
Aidha alisema katika
sherehe hizo wazee 25,000 waliofikia umri wa miaka 70 na kuendelea,watapatiwa
vitambulisho vitakavyowasaidia katika kupata huduma mbalimbali za kijamii
ikiwemo kupokea pencheni jamii, kupata huduma za afya, kuingia katika viwanja
vya michezo vya Serikali pamoja na kutumia usafiri wa daladala bure.
“Wizara ya Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepanga kutoa vitambulisho 25,000 kwa wazee
wote waliofikia umri wa miaka 70 na kuendelea, ili viweze kuwasaidia katika
kupata huduma mbali mbali za kijamii ikiwemo kupokea pencheni jamii, kupata
huduma za afya, kuingia katika viwanja vya michezo vya Serikali, kutumia
usafiri wa daladala bure, nk.” Alisema Waziri Pembe
Alifahamisha kuwa wizara
itaendelea kuimarisha hali za wazee hao ikiwa ni pamoja na kuwapima maradhi
mbalimbali mara kwa mara ili kuchukuwa hatua pale mabapo itatokea mmoja wapo
atakutwa na ugonjwa wowote hivyo kupitia maadhimisho hayo wizara imeandaa
wataalamu wa afya watakao huduma za vipimo vya maradhi mbalimbali bure kwa
wazee na wananchi wote.
“Wizara ya Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeandaa wataalamu wa afya ili wazee na wananchi
wote waweze kupimwa afya zao bure kwani afya bora ndio mtaji” Aliongezea
Kila ifikapo Oktoba 01,
dunia huadhimisha siku ya wazee duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Uthabiti
wa Wazee kwenye Dunia yenye Mabadiliko”
0 Comments