Na Ahmed Abdulla:
IKIWA
imezoeleka kwa miaka ya hivi karibuni visiwani Zanzibar hasa kisiwa cha Unguja
kuzuka tabia ya baadhi ya watu wenye ulemavu kukaa barabarani na wengine
kutembezwa katika mitaa kwa ajili ya kuombaomba.
Jambo
hili limeibua hisia za watu mbalimbali ikiwemo jumuiya zisizo za kiserikali kwa
kuanza kulitafutia ufubuzi jambo hilo na kuwafanya watu wenye ulemavu kuwa na
shughili za kujiingizia kipato na kuondokana na dhana hiyo.
Miongoni
mwa jumuiya hizo ni chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania Upande wa Zanzibar
TAMWA-ZNZ ambapo wameshindikiana na shirikisho la jumuiya za watu wenye ulemavu
zanziba SHIJUWAZA ambapo wanapigana kwa hali na mali ili kuona maisha ya watu
wenye ulemavu si tegemezi.
Nairat
Abdallah Ali ni Afisa uwezeshaji wanawake kiuchumi kutoka chama cha waandishi
wa Habari wanawake Tanzania TAMWA-Zanzibar amesema katika kuhakikisha wanafikia
makundi mbalimbali ya watu wenye ulemavu wanatekeleza mradi jumuishi wa kuwawezesha
watu wenye ulemavu kiuchumi (KIJALUBA Isave)
Amesema
mradi huo wa miaka miwili una lengo la kuinua thamani ya watu wenye ulemavu kwa
kuwawezesha watu wa jamii hiyo kiuchumi.
“lengo
la mradi huu ni kuwafanya watu wenye ulemavu waweze kujitegemea kiuchumi,kuwa
na shughuli za kufanya za kujiingizia kipatao pamoja na kuwa na akiha” amesema
Afisa huyo
Amesema
kupitia mradi huo huendesha mafunzo kwa watu wenye ulemavu yanayolenga kuwawezesha
watu wenye ulemavu kufanya biashara ili kujikwamua kiuchumi kutokana na kundi
hilo kuonekana lipo nyuma kimaendeleo.
Amesema
mradi huo unatekelezwa kwatika wilaya mbili ambazo ni wilaya ya Kusini Unguja
na Wilaya ya Chakechake Pemba na una jimla ya vikundi 43 na awamu ya kwanza
waliwapa mafunzo ya kuweka na kukopa huku kwa awamu ya pili mafunzo
yanawafundisha juu ya utambuzi na usimamizi wa biashara yaliyofanyika katika
ukumbi wa walimu Kitogani wilaya ya Kusini Unguja.
“Awamu
hii ni kubwa na muhimu kwani ili mtu aendelee kuweka akiba lazima awe na
biashara ya kudumu” ameongeza
Kwa
upande wao baadhi ya watu wenye ulemavu wilaya ya Kusini Unguja wamesema mafunzo
ya mbinu za kufanya biashara yatawasaidia kuwaonesha njia za kuzifikia fursa za
kujiingizia kipato na kujikwamua na umasikini unaoelekea kwenye utegemezi.
Mohammed
Ali ni Mkaazi wa kijiji cha Paje yeye ana ulemavu wa uoni amesema awali alijuwa
biashara ni kuuza na kuniniwa tu ila baada ya mafunzo hayo amejifunza ya
kuchagua biashara,kupanga gharama,kupanga matumizi pamoja na masoko.
“natarajia
kuanzisha biashara ambayo imezingatia vipengele vyote nilivyofundishwa na nina
ibami itakuwa endelevu” amesema Mohammed
Kwa
upande wa Zawadi Ali Suleiman mkaazi wa Mzuri Makunduchi ambaye ana ulemavu wa
viungo amesema kupitia mafunzo hayo yatamuwezesha kuongeza ufanisi katika
uendeshaji wa biashara zake ndogondogo.
“kwa
sasa nafanya biashara zangu ndogondogo kama kuuza juisi na malai pamoja na
kutekeleza kazi za shamani ila mafunzo haya yataleta mabadiliko kwangu na
familia yangu” amesema mwanamama huyo
Mkufunzi
wa mafunzo hayo Muhidini Ramadhan Muhidini
ambaye ni afisa muwezeshaji wa masuala ya biashara na vikundi amewasisitiza
wasimamizi hao wa vikundi wanapotaka kuanzisha biashara zao kuwa na malengo ikiwemo
kujua faida , hasara na mitaji, soko na kudhibiti matumizi ya familia ili kuwa
na biashara nendelevu.
Alisema
vingi vingi havifikii malengo kutokana na kutokuwa na mipango Madhubuti ya
kuendesha biashara zao.
“vikundi
vingi vinakufa kwa kutokufuata utaratibu na miongozo ila kama utaifata miongozo
hii biashara au kikundi kitadimu na kuwa na tija” amesema Mkufunzi huyo
Mafunzo
hayo ya siku mbili kwa viongozi na wasimamizi wa vikundi jumuishi vya kuweka na
kukopo wilaya ya kusini yameandaliwa na TAMWA Zanzibar ikiwa ni utekelezaji wa
mradi huo.
0 Comments