Na Nafda Hindi:
WAHARIRI wa vyombo mbalimbali vya habari wametakiwa kutumia nafasi zao kuwasaidia waandishi wa habari vijana kwa lengo la kuleta maendeleo nchini.
Akizungumza na wahariri Mkurugenzi wa TAMWA,ZNZ
Dk Mzuri Issa amesema wahariri wana nafasi kubwa ya kuwaongoza na kuwaelekeza
waandishi vijana katika utendaji wa kazi
zao ili waweze kuleta tija kwa jamii na taifa kwa Ujumla.
Dk Mzuri amesema katika kuhakikisha vijana
wanafanyakazi nzuri lazima wahariri
watowe mashirikiano ya kutosha na kuwaonesha njia ambazo zinaweza kuwasogeza
mbele katika kuleta maendeleo kwa mtu mmoja moja na Taifa kwa ujumla pamoja na
kuiletea sifa nchi ya Zanzibar.
Aidha amewasihi waandishi wahabari vijana
kuwaheshimu viongozi wao wa Taasisi na kufanya kazi kwa mashirikiano ya pamoja
kwa lengo la kujifunza na kuchota ujuzi zaidi kutoka kwao.
Mapema Afisa anaeshuhulikia mradi wa kuwaezesha
waandishi wahabari vijana Tatu Mtumwa amewahakikishia wahariri wa vyombo vya
vyombo vya habari kuwashirikisha ipasavyo kuwasaidia vijana katika kazi zao za
Uandishi ili kufikia malengo yaliokusudiwa.
Nao wahariri kutoka vyombo tofauti wamesema wana
kazi ya ziada ya kuzipitia na kuzifanyia masahihisho habari wanazoletewa katika
vyumba vyao vya habari hivyo wamewaomba waandishi wahabari vijana kujituma na
kusikiliza miongozo sahihi unayopewa na waliokutangulia katika fani hiyo.
Afisa Ufatiliaji na Tathmini kutoka TAMWA,ZNZ
Mohamed Khatib Mohamed amewaomba wahariri wa vyombo vya habari waandae
utaratibu maalum wa kufatilia habari zinazotoka kupititia vyombo vyao vya
habari zinaleta mabadilko katika jamii.
Salim Said Salim ambae alikuwa ni Jaji Mkuu wa
kuzipitia na kuzichambuwa kazi za waandishi vijana zilizoshindaniwa katika
Tunzo ya kuandika habari za wanawake na Uongozi amesema baadhi ya kazi zilizopelekwa
kushindaniwa hazikuwa na vigezo hivyo ni jukumu la wahariri kuzipitia kwa kina
na umakini wa hali ya juu habari ambazo zinawasilishwa katika vyombo vyao.
Imane Duwe ni Mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha
Taifa cha Zanzibar {SUZA) Idara ya Mawasiliano amesma ni vyema kwa Chama cha
Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA.ZNZ kuandaa mafunzo maalum kwa waandishi
wahabari wanawake namna ya kuweza kutumia vifaa kama vile vifaa vya kurikodia
sauti na picha wakati wa kuandaa kazi zao
Hata hivyo waandishi wahabari vijana wamesema
wanakabiliwa na changamoto kadhaa wakati wa kutayarisha kazi zao ikiwemo
mashirikiano madogo kwa baadhi ya vyanzo vya habari wakati wa kukusanya taarifa
na kwenda kuzifanyia kazi.
Mkutano huo wa siku moja uliwashirikisha
wahariri wa vyombo mbali mbali vya habari kutoka Zanzibar pamoja na waandishi
wahabari vijana wenye lengo la kushajihisha waandishi kujikita zaidi kuandika
habari za wanawake na Uongozi ulioandaliwa na TAMWA.ZNZ kwa kushirikiana na
Ubalozi wa NORWAY.
0 Comments