Nafda Hindi , Zanzibar
Katika
kuhakikisha kwamba watu wenye ulemavu wanaondokana na utegemezi TAMWA ,ZNZ kwa kushirikiana
na Shirikisho la J umuiya ya watu wenye ulemavu Zanzibar (SHIJIWAZA) wameandaa
utaratibu maalum wa kukusanya vikundi vya Ushirika kwa watu hao venye lengo la kuweka
na kukopa na kupata akiba itakayowawezesha kutatua matatizo madogo madogo
yanayowakabili katika hali ya kiuchumi.
Watu
wanaoishi na ulemavu ni miongoni mwa wanufaika wakubwa wa mradi wa Kijaluba
Isave unatekelezwa kwa majaribio katika Wilaya ya Kusini kwa Unguja na Chake
Chake kwa Pemba Maafisa mradi wa KIJALUBA ISAVE kutoka TAMWA,ZNZ wamepata
nafasi ya kuvitembelea vikundi hivyo katika Wilaya ya Kusini Unguja kwa lengo
la kutoa taaluma juu ya masuala ya kuweka na kukopa pamoja na sheria zake
zitakazo waongoza kufikia malengo yao waliojiwekea.
Vikundi
vilivyotembelewa ni pamoja na TUSHIKAMANE kutoka Muungoni chenye wanachama 19
wanawake tisa (9) na wanawake kumi na moja(11), TUJIGOMBOWE, kutoka Nganani
Makunduchi, chenye wanachama ishirini na mbili (22) wanawake kumi na tisa (19)
na wanaume watatu(3) na JUMUISHO
kutoka
Nganani chenye wananchama ishirini na nne(24) wanawake ishirini (20) na
wanaume
wanne (4). Vikundi vyote hivyo vilivyofikiwa na Maafisa Miradi kwa pamoja
wamesema vinakabiliwa na changamoto ya uelewa mdogo kuhusu masuala ya utunzaji
wa fedha ikizingatiwa kwamba katika ushirika sekta hiyo ni njeti inayohitaji
taaluma ya hali ya juu.
“Tumeanza
katika vikundi lakini bado hatuna Elimu yeyote kuhusu utunzaji wa fedha kwa
hiyo tunahitaji taaluma hiyo ili tuweze kusonga mbele harakati za uwendeshaji
wa vikundi,” alisema Amina Haji Seti, mshika fedha kutoka kikundi cha JUMUISHO,
Mapema
msimamizi wa vikundi kutoka ukanda wa Makunduchi Is haka Mohammed Kheri amesema
utunzaji wa fedha ni kikwazo kinachowasumbuwa wana vikundi katika ujazaji wa
taarifa zao na kugundua mapungufu kadhaa ambayo yanahitajika kufanyiwa
marekebisho.
“Katika
suala la ujazaji katika masuala ya fedha tunagunduwa makosa mengi na ii inatokana
na wahusika kutokuwa na taaluma ya kutosha katika eneo hili,” alisema Maalim
Is-haka.
Hata
hivyo alizungumzia suala la kuoneana muhali kwa upande akutonzana faini katika
sheria za adhabu ni jambo linalojitokeza katika vikundi vya Ushirika wakati fedha
zinazoingia za faini ndio sehemu ya mfuko wao wa mkopo.
Mradi
wa KIJALUBA ISAVE inwaotekelezwa kwa pamoja na TAMWA.ZNZ kwa kushirikiana
Shirikisho la Jumuiya ya watu wenye ulemavu Zanzibar (SHIJIWAZA) ni mradi wa
majaribio katika Wilaya mbili, Kusini kwa Unguja na Chake Chake kwa Pemba.
0 Comments