Na
Nafda Hindi, Zanzibar
Madaktari nchini wametakiwa kutoa huduma bora
kwa jamii ili kupunguza idadi ya vifo kwa watoto na mama wajawazito.
Ushauri huo umetolewa na wanawake ambao ndio
walengwa wakuu wa kupokea huduma za Afya ya Uzazi kutoka maeneo tofauti visiwani
Zanzibar ambapo wamesema katika vituo
vinavyotowa huduma hizo bado kunahitaji nguvu za ziada kwa madaktari wanaoshughulikia
huduma ya afya ya uzazi.
Wamesema kuna changamoto kadhaa ambazo
zinajitokeza wakati wa kupokea huduma ikiwemo uelewa mdogo kwa madaktari
kuhusiana na afya ya uzazi jambo ambalo huleta shida kwa wanawake endapo
watajiunga na moja ya huduma hizo wakati wa kutumia.
“Huduma za Afya ya Uzazi Zanzibar bado ni
kikwazo hawa madaktari wenyewe yawezekana hawana Elimu sahihi juu ya afya ya
uzazi, kwa mfano Uzazi wa mpango, huangaliwi Afya yako, Uzito wako na
kushauriwa njia ipi sahihi utumie kwa mujibu wa Afya yako unajikuta unapewa
vidonge au sindano kumbe haviendani na afya yako hivyo baadae vinaleta matatizo,”walisema
wananchi.
Mapema Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Taifa
(SUZA) Dk Said Khamis akiwasilisha ripoti ya Afya ya uzazi amesema “chanagamoto
ni nyingi kwa jamii kuhusu Afya ya uzazi kwa sababu inaonekana Zanzibar hakuna
wataalam wa Afya ya uzazi,” alisema Dk Said.
Dk Said amesema waandishi wa habari nao wana
uelewa mdogo kuhusu Elimu ya Afya ya uzazi Zanzibar ipo haja kwa Serikali na
Mashirika binafsi kuekeza nguvu katka masuala haya na kuwapatia mafunzo
waandishi wa habari kwa lengo la kuelimisha jamii.
“Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa unaonesha
kwamba 60% ya vyombo vya habari Zanzibar hakuna vipindi vinavyohusu Afya ya
Uzazi,” Dk Said alisema.
“Tunauelewa mdogo kuhusu Elimu ya afya ya uzazi
kwa sababu sisi tunaelimisha jamii kupitia vyombo vya habari tutakapokuwa na
Elimu sahihi na jamii itajifunza kitu kupitia kwetu, sasa tunahitaji kupatiwa
mafunzo juu ya suala hili,” waandishi wahabarin walisema.
Afisa anaeshughulikia Mradi wa Afya ya Uzazi
kutoka TAMWAupande wa Zanzibar Zaina Abdalla Mzee amesema changamoto ni nyingi kuhusu
Afya ya Uzazi hivyo waandishi wahabari wana kazi ya ziada na kuhakikisha
wanatoa Elimu kwa usahihi kwa kutumia takwimu na kuwafuata wataalam.
0 Comments