Na Nafda Hindi,Zanzibar
Licha ya serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo kuhamasisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi lakini bado kuna changamoto ya upatikanaji wa huduma hizo hususan za afya ya uzazi.
Akiwasilisha ripoti ya awali ya tathmini kwa vyombo vya Habari juu ya kuripoti masuala ya haki ya afya ya uzazi (SRHR) kwa wasichana na wanawake wa mjini na vijijini uliofanywa na chama cha waandishi wa Habari wanawake Tanzania TAMWA Zanzibar hivi karibu, juu ya kuwajengea uwezo waandishi wa Habari kuripoti taarifa za afya ya uzazi kwa usahihi, mhadhiri wa chou kikuu cha taifa Zanzibar SUZA dk Said Mohammed Khamis amesema utafiti huo umebaini uwepo wa changamoto mbalimbali katika upatikanaji wa huduma hizo.
Amesema kwa mujibu wa utafiti huo umeonesha kuwa miongoni mwa changamoto ni Pamoja na uwelewa mdogo kwa jamii, kutokuwepo kwa usiri,mila, silk ana tamaduni, masafa marefu ya kufuata huduma, lugha mbaya kwa baadhi ya watoa huduma ambavyo vinarudisha nyuma wanachi Kwenda kupata huduma hiyo.
Dk Said amefahamisha kuwa miongoni mwa waliohojiwa asilimia 42 wamesema wanapoteza muda mrefu kuisubiri huduma hiyo, asilimia 21 walisema watoa hudumma sio rafiku na asilimia 14 walifahamisha kuwa hakuna usiri katika kupokea huduma hiyo.
“Utafiti uliofanywa ulionesha kwamba asilimia 74 ya wanawake huenda pekee yao katika vituo vya afya ambapo hali hiyo inaonesha wazi kwamba kuna mashirikiano madogo kwa wanaume kuwapeleka wake zao Kwenda kupata huduma hiyo,” Dk Said alisema.
Mbali na hayo alisema asilimia 49 ya waliofikiwa na utafiti huo walisema elimu ni ndogo kwa jamii juu ya afya ya uzazi.
Akizungumzia waandishi wa Habari alishauri kujengewa uwezo waandishi wa Habari ili kupata uelewa na uwezo wa kuripoti taarifa za uzazi wa mpango kutokana na sababu mbalimbali.
“Kati ya changamoto zilizoonekana katika utafiti huo ni Pamoja na elimu duni Pamoja na upatikanaji wa taarifa hizo hukabiliwa na vikwazo pale wanapokwenda kwa wahusika,”Dk Said alisema.
Hata hivyo alifahamisha kuwa takwimu za utafiti huo zinaonesha kwamba asilimia 47.6 ya waandishi wa Habari wanauelewa mdogo kuhusu afya ya uzazi, huku asilimia nne wanauelewa mzuri na asilimia 23 hawaelewi kabisa, haliambayo hawatoweza kufanya kazi zao kwa ufanisi juu ya kuielimisha jamii kuhusiana na suala hilo.
Sambamba na hayo alifahamisha kuwa katika utafiti huo alisema asilimia 38 ya waandishi wa Habari wamepata mafunzo huku asilimia 41 ya waandishi hao hawajapata taarifa za afya ya uzazi hivyo kutokana na hali hiyo ipo haja ya kwa waandishi kupatiwa mafunzo hayo ili kuweza kutekeleza kazi zao kwa ufanisi.
Aidha alisema Zanzibar ni miongoni mwa nchi iliyoridhia mikataba mbalimbali ya kimataifa ambayo inafuata sera na sheria ambapo kwa mujibu wa dira ya 2020 inazungumzia usawa wa masuala ya kijinsia sambamba na masuala ya udhalilishaji, hivyo kutokana na hali hiyo ipo haja ya kuwekewa mikakati Madhubuti juu ya kuripoti taarifa hizo kwa maslahi mapana ya nchi.
“ Jamii inahitaji kuelimishwa Zaidi juu ya umuhimu wa afya ya uzazi kwa maslahi mapana ya kuimarisha ustawi wa afya zao ili kuwa na taifa bora litakaloweza kupigania haki za kiuchumi, kijamii na kisiasa hatua ambazo zitasaidia kuchochea upatikanaji wa maendeleo,” Dk Said alisema.
Nae Ofisa Ufatiliaji na Tathmini, Mohamed Khatib Mohamed alisema mradi huo unalengo la kuwajengea uwezo waandishi wa Habari kuripoti taarifa za afya ya uzazi ili kuongeza uelewa kwa jamii kutumia huduma hiyo masilahi mapana ya nchi.
“Waandishi wahabari ni kioo cha jamii hivyo Elimu wanayopewa ni lazima waitumie kuifikisha kwa jamii kwa kutumia kalamu zao kwa kuandika,kuripoti na kutayarisha vipindi kwa lengo la kufikisha ujumbe,” Afisa Ufatiliaji na Tathmini Tamwa,ZNZ alisema.
Washiriki wa mkutano huo walishauri waandishi wa Habari wanapofanya kazi hiyo ni vyema kuchagua lugha iliyosahihi isiyoleta madhara kwa jamii ambayo itaweza kulinda mila, silka na destuli za wazanzibari.
“Lugha inayotumika sasa hivi katika vyombo vya habari ni mtihani, imefika wakati unatizama TV ukumbuni pamoja na familia yako unashindwa inabidi uondoke kwa sababu kila Taifa linaangalia utamaduni wao, hivyo vyombo vya habari vinaporusha au kutangaza vipindi lazima wazingatie mila,desturi,silka na utamaduni wa Mzanzibari,” Bi Asha Aboud alisema.
Tamwa Zanzibar inatekeleza mradi wa SRHR kwa kushirikiana na Tamwa Tanzania bara,,,, kwa lengo la kupunguza vifo vya mama wajawazi na Watoto Utafiti huo uliwashirikisha watu 102 kati ya hao wanawake walikuwa asilimia 36 na wanaume asilimia 37, huku vyombo vya Habari vilivyofikiwa na utafiti huo vilikuwa asilimia 21.
0 Comments