Na Nafda Hindi
Wanawake wenye nia ya kugombea nafasi za Uongozi
wameaswa kutovunjika moyo licha ya matatizo kadhaa wanayokumbana nayo katika
kufikia malengo waliyokusudia.
Akizungumza na wanawake kutoka vyama mbali mbali vya
siasa mratibu kutoka TAMWA Maryam Ame Choum amesema wanawake kwa sasa
wamewawezesha wanawake zaidi ya thamannini kutoka Unguja na Pemba kwa kuwapa
mafunzo ya kuwajengea uwezo katika kugombania nafasi za Uongozi.
Mapema Katibu Mwenezi CCM Khamis Mbeto amesema wanawake
wana uwezo wa kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja hivyo wapewe nafasi za
Uongozi kwa kuzingatia vigezo na utendaji wao wa kazi.
“Chama cha Mapinduzi kinatambuwa uwezo wa wanawake
katika utendaji wao na mfano mzuri ni Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na anafanya vizuri , kwa kweli wanawake wapewe nafasi kwa kuzingatia
uwezo, sifa na vigezo”, alisema.
Nae Katibu Mkuu CHADEMA Taifa Salim Mwalim amesema
kwa sasa wakati umefika kuongeza idadi ya wanawake katika ngazi za maamuzi bila
kuathiri mila,silka na utamaduni wa Mzanzibari.
“Wanawake kiwango chao cha uaminifu ni kikubwa ukilinganisha
na wanaume, hivyo tunaweza kuwa na viongozi wanawake na tukalinda mila,silka na
desturi ya Mzanzibari,”alisema.
Halima Ibrahim kutoka chama cha ACT Wazalendo amesema
wanawake wamekuwa wakikabiliwa na changamoto kadhaa wakati wakugombea nafasi za
uongozi ikiwemo rasilimali fedha hivyo amewaomba wanawake wenye nia ya kugombea
washirikiane kwa pamoja kwa lengo la kumkombowa mwanamke.
“Wanawake wenzake tunakabiliwa na changamoto kadhaa
katika haya mambo hivyo wasia wangu kwangu tuungane pamoja ili kumkombowa
mwanamke bila kuangalia itikadi za vyama.ukabila,rangi,dini wala mtu alipotoka,”alisema.
Nao washiriki wa mkutano huo wamesema katika kufikia
ngazi za maamuzi kuna matatizo kadhaa wanayokutana nayo ikiwemo mfumo uliwekwa
katika vyama vya siasa na jamii kutokubadilika kwa kuwa na dhana potofu kuwa
mwanamke hawezi kuongoza.
0 Comments