Mbunge wa wananchi wa Jimbo la Chumbuni (CCM) Ussi
Salum Pondeza ameambatana na Maafisa waandamizi wa Jeshi la Polisi Tanzaniakulitembelea
na kulikagua eneo lililo kuwa kituo
kidogo cha polisi Chumbuni ili kujiridhisha kuwa ni sehemu sahihi ya kujenga
kituo kipya Cha polisi.
Azma ya ujenzi wa kituo hicho ni kukizi
mahitaji ya wananchi wa Jimbo hilo na
maeneo jirani, na ikijulikana kuwa eneo hilo ni karibu na hospitali ya Wilaya iliyopo Chumbuni.
Hatua hiyo ya Kutaka kuanza kwa ujenzi Wa kituo
hicho ni Kufuatia maelezo ya Mbunge Pondeza Kupitia Wizara ya Mambo Ya Ndani Ya
Nchi kwenye vikao vya Bunge Jijini
Dodoma.
Ujenzi huo unaotarajiwa kuanza hivi karibuni Chini
Ya Wizara Ya Mambo Ya Ndani Ya Nchi Na
Nguvu Ya Mbunge Wa wananchi Wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza .
0 Comments