Ticker

6/recent/ticker-posts

CMSA Yawafumbua Macho Wajasiriamali Zanzibar Upatikanaji Mitaji Halaiki

Mkurugenzi Mkuu SMIDA, Soud Said Ali Akifungua mafunzo Kwa Wajasiriamali Na Wakufunzi Ya Namna Ya Kukusanya Mitaji Ya Halaiki Yaliyoandaliwa Na CMSA


Na Ahmed Abdulla:

Mkurugenzi mkuu wa wakala wa maendeleo ya viwanda vidogovidogo, vidogo, na vya kati Soud Said Ali amesema uanzishwaji wa jukwaa la   mitaji ya halaiki itawasaidia wajasiriamali wengi ambao hawajakidhi kupata mitaji katika taasisi za kifedha kupata mitaji kupitia jukwaa hilo ili kuendeleza harakati zao za ujasiriamali.

Aliyasema hayo katika mafunzo kwa wjasiriamali na wakufunzi ya namna ya kutumia hilo kwa lengo la kujipatia mitaji kutoka kwa wananchi ili kuwe na mafanikio ya pande zoned mbili.

“Tunaelewa kuwa kumekuwa na changamoto kwa wajasiriamali wetu kupata mitaji kwenye sekta za kifedha kwa kukosa sifa za upatikanaji wa mitaji hiyo lakini kupitia mitaji hii ya halaiki watafahamu juu upatikaniji wa mitaji hii” alisema mkurugenzi huyo


Aidha alisema mpango huo unaofanywa na CMSA ni kuendeleza dhana ileile ya kukuza uchumi wa wajasiriamali wa Zanzibar kwa uwawekea mazinira ya upatikanaji wa mitaji.  

Akitoa ufafanuzi juu ya mtaji hayaiki mwakilishi wa mamlaka ya masoko ya mitaji na dhamana CMSA, Chales Shirima alisema mitaji halaiki ni ile inayotolewa na wananchi kwa ajili ya kuendesha biashara na kugawana faida.

“mitaji ya halaiki ni migeni hapa Zanzibar na hata Tanzania Bara kwa hiyo tumekuja kutoa elimu ili washiriki na wahitaji mbalimbali waweze kutambua namna wanavyoweza kukusanya mitaji kutoka kwa umma” Alisema Chales Shirima


Mwakilishi wa mamlaka ya masoko ya mitaji na dhamana CMSA, Chales Shirima akitoa ufafanuzi juu ya mitaji halaiki

Kwa upande wao washiriki wamafunzo hayo walisema endepo mitaji hiyo itapatikana itawawezesha kupandua biashara zao pamoja na kuzalisha ajira nyingi zitokanazo na shughuli zao wanazozifanya.

“tunakuwa na changamoto nyingi na kubwa ni kukosa mitaji ya uendeshaji wa shughuli zetu ila ni matarajio yetu hawa CMSA watatusaidia kupata hii mitaji” Alisema mmoja wa washiriki

Post a Comment

0 Comments