Ticker

6/recent/ticker-posts

Holding Hands Foundation Yachagiza Furaha Ya Watoto Yatima




Serikali ya mkoa wa Kusini Unguja imesema itaendelea kushirikiana na Jumuiya na mashirika yasiyo ya kiserikali ili kukuza ustawi wa jamii za mkoa huo.


Hayo yameelezwa na Mkuu wa wilaya Kusini Rajab Yussuf Mkasaba kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja katika hafla ya chakula cha mchana na watoto yatima iliyoandaliwa na Jumuiya ya Holdin Hands Foundation huko katika ukumbi wa Dkt. Ali Mohammed Shein Tunguu.

Amesema jumuiya na mashirika yasiyo ya kiserikali kwa sasa yamekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono juhudi za serikali zote mbili katika kuhakikisha wananchi wanafikia na huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo Elimu,Afya pamoja bna huduma yamaji safi na salama.

Hata hivyo mkuu huyo wa wilaya amiomba jumuiya ya Holding Hands kufikiria njia mbadala ya kuwasaidia watito hao pamoja na watu wenye mahitaji maalumu ikiwa ni pamoja na kuwafungulia acounti za benk pamoja na wawekea fedha zitakasowasaidia katika siku za usoni.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Holding Hands Foundation Florance Robert amesena lengo la hafla hiyo ni kuwaonyesha upendo watoto hao ili wasijihisi kuwa wametengwa na jamii.

Amesena mbali na kuwasaidia watoto yatima katika eneo hilo lakini pia wanawapatia bima ya afya pamoja na kuwalipia gharama za masomo watoto hao na wale wenye mazingira magumu.

Nao watoto hao wameipongeza Jumuiya hiyo kwa kukaa nao pamoja kupata chakula hicho huku wakiiomba kuendelea kuwasaidia katika maeneo mingine.

Jumla ya watoto 300 wamejumuika pamoja katika hafla ya chakula hicho.

Post a Comment

0 Comments