Wananchi wa maeneo ya Jambiani Paje na maeneo Jirani wanatarajiwa
kuondokana na tatizo la ukosefu wa maji safi na salama mara baada ya kukamilika kwa zoezi la ufungaji wa vifaa vya
kuongezea nguvu za umeme katika
visima vya Jambiani Kumbini na Paje.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini
Unguja Mhe Rashid Hadid Rashid ameyasema hayo wakati akifanya ziara na
watendaji wa mamlaka ya maji zawa, shirika
la umeme ZECO, na uongozi wa wilaya na
jimbo ikiwa ni muendelezo wa taasisi hizo kufanya ukaguzi katika vianzio vya maji ili kubaini
matatizo yanayosababisha kukosekana kwa huduma hiyo kwa baadhi ya maeneo ya
mkoa huo.
Amesema mara baada ya kufanyika ukaguzi na watendaji hao kumebainika kueko kwa tatizo la umeme mdogo Pamoja na
kutobolewa kwa miundo mbinu kiholela kwa shughuli za kilimo hivyo amewataka
wananchi kuachana na tabia hiyo sambamba na kuwataka watendaji wa taasisi hizo
kuharakisha zoezi la ufungaji wa vifaa hivyo ili wananchi waweze kuondokana na
usumbufu wanaoupata hasa katika kipindi hichi ambacho tunaelekea na mwezi
mtukufu wa Ramadhani.
Nao wataalam
kutoka mamlaka ya maji zawa
mkurugenzi ufundi injinia Hassan khamis Hassan
na injinia wa zeco Ali Kassim wamesema watahakikisha wanalisimamia zoezi hilo ili kuona huduma hiyo inapatikanwa kabla ya mwezi
mtukufu wa Ramadhan huku wakiwasisitiza
wananchi kuitunza na kuilinda
miundombinu ya huduma hizo ili
kuipunguzia hasara Serekali.
Nae kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Paje Mhe Jaffar Jussa
Sanya amesema uongozi wa jimbo hilo
utaendelea na juhudi zake za kuzitafutia
ufumbuzi changamoto zinzowakabili wananchi katika huduma muhimu ikiwemo maji, afya, na elimu.
0 Comments