Bi Salma Sadat. |
Na Ahmed Abdulla
Wadau mbali mbali wa
haki za watu wenye ulemavu wamesema ipo haja kutazamwa tena sheria hiyo kwani
kuna baadhi ya changamoto ambazo zinaonekana kuhitaji mabadiliko.
Wameyasema hayo wakati
walipokua wakizungumza na mwandishi wa habari hizi alietaka kujua kama wameona
mapungufu ya sheria hizo ili ziweze kufanyiwa kazi.
Mmoja wa wadau hao
ambao ni Mkurugenzi wa Baraza la watu wenye ulemavu Zanzibar Bi Salma Sadat
alisema vipo vipengele vingi vya sheria ambavyo vinahitaji kufanyiwa maboresho.
Akivitaja vipengele
viyo Bi Salma alisema alisema ni pamoja kipengele na 42 ambacho kimesema ‘’mtu
yoyote atake mficha mtu mwenye ulemavu
atakua ametenda kosa akitiwa hatiani atalipa faini shilingi elf hamsini
au isiozidi laki tano za kitanzania. ‘’
Bi Salma anasema hukumu
hii ni ndogo sana kulingana na mazingira halisi,jamii inapaswa kutambua kuwa
kumficha mtu mwenye ulemavu ni kumnyima haki zake za msingi ikiwemo kupata
elimu.
Alisema mtu mwenye
ulemavu ni sawa na mtu mwengine hivyo anapaswa kupata haki zote za msingi kama
mtu mwengine.
Alisema wamekua
wakipokea kesi ambazo si kwa kiasi kikubwa bado baadhi ya wazazi na walezi
wamekua wakiwaficha watu wenye ulemavu majumbani mwao jambo ambalo alisema
linapaswa kulaaniwa na kupingwa vikali.
Mmoja miongoni mwa
mzazi ambae mtoto wake ana ulemvu anaeishi kisauni Wilaya ya Magharib B Unguja
Rashid Maalim aliwataka wazazi na walezi wenzake kuacha kuwafungia watu wenye
ulemavu majumbani.
Alisema kuwafungia watu
wenye ulemavu majumbani ni kitendo kibaya pia kinapingwa na dini zote kwa
sababu hivyo hakina budi kuachwa na jamii kubalika.
Kupitia vyombo vya
habari miezi kadhaa nyuma iliripotiwa habari katika kituo cha ZBC kipindi cha
mawio ambacho kilifichua mtoto anaeifichwa ndani na kuleta mshangao mkubwa kwa
jamii.
0 Comments