IMEANDIKWA NA SWALEH SHRIMP:
Mikel Arteta alikutana Josep Sala akiwa na umri wa miaka 15 huko Catalunya na Uhispania Kati yao ulianza kujengwa huko muda ukapita Mikel alitangulia Uingereza akiwa Mchezaji huku Guardiol yeye alibaki Uhispania.
Pep Guardiola Wakati anamalizia maisha pale Ujerumani aliwasiliana na Arteta ambaye kwa wakati huo alikuwa yupo Uingereza na kumuelezea Kama ana ndoto ya kufanya kile alichokifanya akiwa Barcelona kwenye ligi aje kukifanya Uingereza .
Guardiol alimwambia Arteta "Nafahamu Kama unaona ni ngumu na haiwezekani hata wengeni wanahisi Hivyo Lakini nakuomba uje kuwa msaidizi wangu ili kunisaidia kufikia ndoto hiyo".
Pep Guardiol alipotuwa Manchester City mnamo mwaka 2016, alimwambia Sheikh Mansour Kama anamuhitaji Arteta kando yake ili Safari yake isiwe ngumu.
Hapo Mikel Arteta alikuwa amemaliza maisha yake ya uchezaji akiwa na Arsenal, na alikuwa na fursa ya kufanya kazi katika akademi yao, lakini aliamua kumfata Guardiol licha ya kuwa na mashaka kuhusu kuchukua kazi kubwa kama jukumu lake la kwanza katika ukocha.
Arteta alipofika Manchester City alimwambia Guardiol "Sijafundisha mtu yeyote kwa hivyo nitawezaje kuwa Mkufunzi bora zaidi ulimwenguni na kurudisha kitu ambacho unatarajia nifanye?" ndio hapo Pep alimtizama usoni Mikel huku akitabasamu na kumjibu "Nilikuwa nakuhitaji wewe na sio wasiwasi wako hivyo umefika nakushukuru".
Safari ikaanza Pep Guardiol akawa ana kazi mbili akimaliza kuifundisha timu anamchukuwa Mikel Arteta na kuanza kumpa darasa na kesho yake Arteta akawa anafunguwa yeye zoezi la timu.
Guardiol alimwambia Arteta kwamba apendelee kusikilizi Sana kwa umakini hii itapelekea kuongea kidogo na kufahamika na hapo wachezaji wa City walikuwa wepesi kumuelewa Mikel akianza kufunguwa zoezi na ikazidisha imani kati yao.
Licha ya Mwaka wa kwanza wa Pep kwenda kinyume na mpango kwani City ambayo ilimaliza msimu wa 2016-17 bila taji lolote lakini Imani ya Guardiol kwa Arteta haikuyumba kwasababu alikuwa na imani Kwamba timu inaelekea katika mwelekeo sahihi.
Arteta alimwambia Pep Guardiol kuwa "Ni muda Sasa wa kuelewa utamaduni wa soka la Uingereza jinsi waamuzi wanavyofanya, jinsi vyombo vya habari vinavyofanya kazi" Basi Walikaa chini na mafaili yote na kilichofata ni HISTORIA tu .
0 Comments