Mwandishi wa habari mwandamizi Zanzibar Salim Said Salim akichangia katika mkutano uliofanyika ofisi za TAMWA-ZNZ Tunguu Wilaya ya kati Unguja. Picha na Muhammed Khamis |
Mkurugenzi wa Chama cha
waandishi wahabari Wanawake TAMWA-ZNZ Dkt Mzuri Issa amesema kuna haja ya
ushirikishwaji kikamilifu kwa waandishi wa habari katika michakato ya uundwaji
ama urekebishwaji wa sheria mbali mbali zinazohusu umma.
Dkt Mzuri ameyasema
hayo katika ukumbi wa Chama hicho Tunguu Wilaya ya kati mkoa wa kusini Unguja
alipokua akizungumza na wadau kutoka taasisi mbali mbali za Serikali na binafsi
katika mkutano wa siku moja uliokua na lengo la kuzitazama na kutoa maoni yao
kwa baadhi ya sheria ikiwemo sheria ya tume ya uchaguzi,sheria ya habari na
sheria ya takwimu Zanzibar.
Alisema kuna baadhi ya
sheria zinazonekana kuleta mkanganyika katika utekelezaji wake huku baadhi ya
sheria hizo zikionekana kuminya uhuru wa habari na waandishi wa habari kufanya
kazi zao kwa maslahi ya Umma.
‘’Ili kuepuka haya ni
vyema sisi waandishi wa habari tukashirikishwa kikamilifu tangu hatua za awali
kwenye uundwaji wa sheria ili kutoa maoni yetu pale tunapoona hapatakua sawa
hususani katika utendaji wetu wa kazi’’aliongezea.
Kwa upande wake
mwanahabari mwandamizi Zanzibar Salim
Said Salim alisema kuna baadhi ya sheria ni za ajabu sana akitolea mfano
kipengele cha sheria ya uchaguzi kinachomkataza mwandishi wa habari
kutojumuisha matukio ya uchaguzi yaliobandikwa vitu vya kupigia kura na maafisa
wenyewe wa tume hiyo.
Alisema kipengele hicho
cha sheria kinakiuka sana uhuru wa habari na kueleza kuwa kuna haja ya
kufanyiwa marekebisho haraka sana ili waandishi wa habari waweze kufanya kazi
zao kwa mujibu wa sheria.
‘’Kwa kuwa maafisa
wenyewe wa tume ya uchaguzi ndio waliojumuisha na kubandika matukio ya kura
kwenye vituo vya kupigia kura huku karatasi hizo zikiwa tayari zimetiwa saini
za wahusika kwanini mwaandishi wa habari azuiwe keshiria kutojumuisha idadi ya
kura husika kutoka kwenye vituo’’alihoji mwanahabari huyo.
Akichangia katika
mkutano huo mwandishi wa habari kutoka shirika la magazeti ya Serikali Tanzania
Bara (TSN) Issa Yussuf alisema ili kuna haja kubwa ya wanaohusika na undwaji na
urekebishwaji wa sheria kuratibu mpango mzima wa kukusanya maoni ya watu kabla
ya kutengeneza sheria ukizingatia wao ndio walengwa wakubwa wa sheria
zinazotungwa hivyo ni wajibu kutoa maoni yao na kuzingatiwa.
Mratib wa Baraza la
habari Tanzania MCT Shifa Said Hassan alisema uwepo wa sheria bora katika Nchi
na umuhimu wa kufuata mikata ya kimataifa ni jambo la msingi na linalopaswa
kutiliwa mkazo zaidi na kila mmoja.
Mkutano huu wa siku
moja umeitishwa na TAMWA-ZNZ kwa kushirikiana na Internews Tanzania uliokua na
lengo la kupitia baadhi ya sheria Zanzibar na kutoa maoni yao juu ya yaleo wanayoona yanahitaji kufanyiwa
marekebisho.
0 Comments