Na Muhammed
Khamis,TAMWA-ZNZ
Chama cha Waandishi wa
habari wanawake TAMWA-ZNZ kimemtaka Msajili wa vyama vya siasa Nchini Tanzania
Jaji Francis S. Mutungi kuangalia
utaratibu utakaovitaka vyama vya siasa Nchini
kubadili vipengele vya katiba za vyama vyao ili kuleta usawa katika nafasi
mbali mbali za uongozi kuanzia kwenye Chama hadi wale wanaopata nafasi kupitia uwakilishi
wa maeneo yao kupitia vyama vyao.
Akizungumza kwa niaba
ya Mkurugenzi wa Chama hicho Dkt Mzuri Issa,Meneja miradi TAMWA-ZNZ Ali Mohamed
alisema licha ya jitihada mbali mbali zinazoendelea kufanywa na wanaharakati
bado wanawake wengi wameshindwa kufikia malengo ya kupata nafasi za uongozi.
Wakati akifungua
mkutano wa majadiliano ya siku moja uliofanyika Tunguu Wilaya ya kati Unguja na
kuwashirikisha wadau kutoka asasi mbali
mbali wenye lengo la kutazama kwa pamoja changamoto za kikatiba za vyama vya
siasa ambazo inaaminika kuwa zimekua miongoni mwa sababu kubwa ya inayowafanya wanawake
kushindwa kutumiza malengo yao.
Alisema ushiriki wa
wanawake katika nafasi za uongozi ni jambo ambalo limekua likisemewa kwa muda
mrefu bila ya mabadiliko yanayoridhisha na anadhani kuwa kitu pekee kilichobaki ni
msajili kuvilazimisha vyama vyote Nchini kubadili vuipengele kwenye katiba zao.
‘’Naamini iwapo katiba
zote za vyama vya siasa vitaweka wazi ushiriki
wa wanawake kwenye nafasi za uongozi litakua suala la lazima na ni wazi kuwa kilio cha wanawake cha muda mrefu
kitamalizika na hatimae wanawake wengi zaidi watashika hatamu za
uongozi’’aliongezea.
Wakichangia katika
mkutano huo baadhi ya washiriki walisema zipo changamoto nyingi ukitoa madhaifu
ya katiba za vyama vya siasa ambazo wanawake wamekua wakikutana nazo kila leo.
Mmoja miongoni mwao
Mohamed Jabir alisema kutoka na mazingira yaliopo sasa inawalazimu wanawake
wanaotaka kushika nafasi za uongozi kujiongeza zaidi kielimu na kuacha hofu.
Alisema kumekua na hofu
kubwa inayowakabili wanawake wengi
wasomi wamekua wakihofia mazingira ya kazi zao au kusubiri kwa muda mrefu huku
wakikosa ajira iwapo wataamua kuingia kwenye siasa za vyama vya upinzani.
‘’Nina wasiwasi mkubwa
hwenda wasomi wengi wataendelea kushindwa kuingia kwenye siasa kutokana na
mazingira kutokua rafiki wengi wao wana hofu kubwa’’aliongezea.
Sambamba na uwepo wa
chanagamoto hizo alisema bado wanawake wana fursa za kuwa viongozi na hawapaswi
kukatishwa tamaa na vikwazo vya aina hiyo.
Nae Hawra Shamte
alisema ili wanawake wengi waweze kushika nafasi kuna haja kila mmoja kuona
suala la wanawake si jambo ambalo linapaswa kuwa wanaume pekee badala yake ni
haki ya msingi ya kila mtu mwenye akili timamu.
Meneja miradi TAMWA-ZNZ Ali Mohamed (katikati)akizungumza na mratib mradi wa kuwawezesha wanawake kuwa viongozi (SWIL) Maryam Ame (kushoto) pamoja na Salma Moulid. |
Mratib mradi wa kuwawezesha wanawake kuwa viongozi Zanzibar ( SWIL ) Maryam Ame akizungumza na washiriki wa makutano wa majadiliano ya siku moja. |
Baadhi ya washiriki wakiendelea na kazi za makundi kabla ya kuwasilisha sababu wanazoamini zinawakwamisha wanawake wengi Zanzibar kutokua viongozi.
|
0 Comments