Na Muhammed
Khamis,TAMWA-ZNZ
Chama cha waandishi wa
habari Wanawake TAMWA-ZNZ kimesema
wakati umefika kwa Zanzibar kuwepo kwa sheria maalumu itakayosimamia baadhi ya maswala yanayohusu dini ya kiislamu ikiwemo ndoa,talaka,mirathi,haki za wanawake pamoja na matunzo
ya watoto ambao wazazi wameachana.
Akifungua mkutano wa
siku moja uliowashirikisha wadau wa taasisi mbali mbali pamoja na viongozi wa
dini mkuu wa miradi TAMWA-ZNZ Ali Mohamed alisema kwa miaka mingi Zanzibar
licha ya kuwa na idadi kubwa ya waislamu lakini imekosa sheria hiyo ambayo wanaamini
kukosekana kwake kunaleta changamoto kubwa ikiwemo baadhi ya wahusika
kutowajibika ipasavyo katika majukumu yao ya kila siku.
Alisema kutokuepo kwa
sheria hiyo imesababisha maswala mengi yanayohusu dini ya kiislamu kuwa na
mkanganyiko mkubwa kutokana na tofauti zinazojitokeza wakati wa maamuzi kutoka
kwa watu wanaowaamini ikiwemo makaadhi na maulamaa.
Alieleza kuwa ili
changamoto hiyo iweze kuondoka ni lazima kuwe na sheria maalumu ambayo
itaelekeza na kusimamia kila kitu namna ya utekelezaji kuhusu uislamu.
Akitolea mfano alisema
baadhi ya wanawake wanaoachika wamekua wakikutana na changamoto kubwa ya kukosa
matunzo yao na watoto wao jambo ambalo dini imeweka wazi namna ya kuwatunza
watoto hata kama wazazi wameachana.
Sambamba na hayo
akifafanua zaidi pia suala la mirathi kwa familia ambazo wazazi wao wamefariki
baadhi ya ndugu zao huamua kufanya wanachoamini wao ni sawa na iwapo imetokea
mmoja kuwa na ugonjwa wa akili huwa hawi sehemu ya wanaopewa mirathi au mali
yake hutumiwa na wengine bila yeye kunufaika.
Akiwasilisha ripoti ya
awali baada ya kuzipitia sheria mbali mbali za kiislamu Zanzibar Mhadhiri
kutoka chuo kikuu cha Zanzibar University Dkt,Sikujua Omar Hamdan alisema
wakati anapitia sheria hizo aligundua changamoto ambazo anaamini zikifanyiwa
kazi Zanzibar itapiga hatua zaidi.
Kwa nyakati tofauti
wakichangia katika mkutano huo baadhi ya wajumbe walisema suala la uwepo wa
sheria lilipaswa kufanyiwa kazi kwa miaka mingi lakini inasikitisha hadi sasa
licha ya uhitaji wa sheria hiyo wenye mamalaka hawajalipa umuhimu jambo hilo.
Mmoja miongoni mwao
Sheikh Nassor Tajo kutoka ofisi ya Mufti Zanzibar alisema sheria ya kaadhi
haikupaswa kubebeshwa maswala ya mtoto au yoyote yale yanayohusiana na maswala
ya kiislamu isipokua sheria hiyo ipo kwa ajili ya kuanzishwa mahkama ya kaadhi
na kutoa mamlaka ya makama hiyo.
Alisema TAMWA-ZNZ
wamekuja na wazo muafaka na wakati sahihi ambapo iwapo sheria hiyo itapatikana
itaipunguzia mzigo mahkama ya kaadhi usiokua walazima.
Nae Mwenyekiti wa
Jumuia ya watu wenye ulemavu Zanzibar (JUWAUZA)
Bi Salma Sadat alisema iwapo sheria hiyo itapitishwa itakua sheria nzuri
na italeta msaada mkubwa kwa jamii.
Hata hivyo alisema
lakuzingatia zaidi ni kuingiza vipengele kwenye sheria hiyo vitakavyohusisha
watu wenye ulemavu ukizingatia kumekua na matukio mengi ya wanawake kutelekezwa
kwa sababu ya kuzaa watoto wenye ulemavu.
Mhadhir kutoka Chuo kikuu cha Zanzibar University Dkt,Sikujua Omar Hamdani alipokua akiwasilisha ripoti ya awali kuhusu changamoto hizo. |
Mhadhir kutoka Chuo kikuu cha Zanzibar University Dkt,Sikujua Omar Hamdani alipokua akiwasilisha ripoti ya awali kuhusu changamoto hizo. |
Picha ya pamoja ya washiriki wa mkutano huo mara baada ya kujadili ripoti ya awali ilioleza changamoto za kukosekana sheri maalumu ya kusimamia mambo yote yanayohusikana na uislamu.
0 Comments