Wanafunzi
wenye lengo la kujiunga na vyuo vya elimu ya juu wameshauriwa kutafuta ushauri kutoka
kwa wataalamu ili kusoma kada wanayoihitaji.
Ushauri
huo ulitolewa na Msaidizi mkufunzi kutoka chuo cha Zanzibar University Nassra
Nassor Suleiman, katika maonyesho maalumu ya chuo hicho yenye lengo la
kuwapatia ushauri wanafunzi wanaohitaji kujiunga na vyuo vya elimu ya juu
kujuwa namna ya ufaulu wao unavyowaweza kujiunga
na kada kulingana na ufaulu huo yanayoendelea katika viwanja vya mnara wa
kumbukumbu ya Mapinduzi, Kisonge.
“Wanafunzi
wanashindwa kutambua kada wanazoweza kusoma kulingana na ufaulu wao” Alisema
Bi, Nassra
Aidha
alisema wanafunzi wengi hupata alama zinazowawezesha kusoma kada zinazohusisha
masomo ya sayansi lakini wanashindwa kutambua hilo na badala yake hujiunga na kada
ambazo hawakuzihitaji.
Sambamba
na hayo amewaomba wanafuzi kufika katika maonyesho hayo ili kupata ushauri huo
pamoja na kupata usajili wa kujiunga na chuo hicho unataotolewa hapo hapo.
“Tunawaomba
wanafunzi wajitokeze hapa kwenye mnara wa kumbukumbu ya Mapinduzi Kisonge ili
wapate ushauri na Kujisajili kwa lengo la kujiunga na chuo chetu” Aliongezea
Bi. Nassra
Kwa
upande wake mratibu wa astashahada na stashahada kutoka chuo hicho Hamed M.
Salum amesema miongoni mwa huduma nyingine zinazopatikana katika maonyesho hayo
ni kuombewa namba ya utambulisho wa stashahada (AVN) pamoja na kufahamishwa kujiunga
na kozi za msingi kwa wale ambao ufaulu wao hauruhusu kujiunga na chuo moja kwa
moja Ambazo zinatolewa na Open University.
0 Comments