Na Ahmed Abdulla:
Wasanii mbalimbali nchini wamesema kuna kila sababu
ya kupantikana kwa uhuru wa kweli wa kujieleza na kupaza sauti za kupinga
ukandamizaji wa haki za wengine ili kupata maendeleo ya kweli nchini.
Wameyasema hayo kwa nyakati tofauti kufuatia kutokuwepo
kwa uhuru wa kweli katika kuyasemea yale yanayowakandamiza watu wa jamii za
chini hali inayohatarisha kuwakosesha haki miongoni mwa jamii za watu hasa wa
tabaka la chini.
Abeid Nasib ni muandishi wa filamu kutoka Zanzibar
amesema uhuru wa kujieleza katika sekta ya filamu haupo kwani maisha halisi ya
Zanzibar yanaleta ukakasi juu ya filamu na ukizingatia kuwa filamu ina uwanja
mpana.
“Filamu ina uwanja mpana hivyo unaweza kuzungumzia
vitu vinavyofanyika Zanzibar lakini ukaambiwa filamu yako imekwenda kinyume na
tamaduni” amesema Abeid
Nilipomuuliza kuhusu uhuru wa kutoa filamu za
kukosoa hapo ndio alisisotiza kuwa haupo kwani ukiangalia tokea enzi za mababu
kuna mengi ambayo yametokezea lakini watunzi wa filamu wameshindwa kutunga
filamu zenye mnasaba wa mambo hayo.
“Kuna mikasa mingi ya siasa iliyojitokeza ya hata
watu kutokuzikana,kuchomeana moto nyumba kwa baadhi ya jamii, ugomvi wa wavuvi
wa jamii moja na nyingine lakini haijawahi kuandikwa filamu ya mambo hayo hivyo
inaonyesha uhuru haupo kabisa” aliongezea
Amesema licha ya hayo lakini bado anayo nia ya
kuandika filamu zinagusa maisha halisi ya
Zanzibar na yale yanayotendeka huku akiwaambia waandishi wenzake kuwa
ili kuleta mabadiliko ya jambo lolote baya basi kuna kila sababu ya kuyaandikia
filamu ili yaonekanwe na jamii nyingine ili yaweze kuachwa.
“Sanaa zinahitaji mambo yanayogusa mioyo ya watu
bila kujali watendaji wataumia kiasi gani kutokana na kuyazungumza mabaya yao”
alimalizia Mwandishi huyo
Bakar Hamad Abdalla kwa jina la sanaa ni Beka-h yeye
nimsomaji wa nasheed kutoka kisiwani Pemba amesema bado uhuru wa kujieleza
umekuwa ni changamoto katika jamii za kizanzibari kwani aliwahi kutoa kazi
inayozungumzia siasa tu kwa ujumla wake lakini baabdi ya vyombo vya habari
walihofia kuicheza.
“Niliwahi kutoa kazi inayozungumzia siasa ila baadhi
ya vyombo vya habari havikucheza kazi hiyo na nadhani ni hofu tu ndio ilifanya
wasiicheze” alisema Beka-h
Amesema licha ya changamoto hiyo lakini haikumfanya
ahofie kutoa kuandaa kazi zinazozungumzia uhalisia wa maisha halisi ya Zanzibar
ambapo kwa sasa anaandaa kazi nyingi zenye kugusa changamoto za wazanzibari.
“Wijahofia bado nitaendelea kutoa kazi nyingi tu
zinazozungumzia maisha halisi ya Zanzibar na changamoto za wazanzibar”
aliongezea
Hata hivyo amewaoma wasanii wenzake na wote wenye
sauti ya kuzunguma wasemee changamoto na kadhia zinazowakabili wananchi ili
wenye dhamana ya maeneo hayo waweze kuwajibika.
Nae msanii wa zenji Fleva Misheli Santiago (Misheli
Tz) naye pia amesema uhuru wa kutoa sanaa inayokosoa watu wa tabaka la juu
haupo na ukizingatia Zanzibar kuna matukio mengi ambayo si ya kawaida.
Amesema watu watabaka la juu wao wanahitaji nyimbo
sa kusifia tu huku watu wa tabaka la chini wao wakihitaji nyimbo zinazowakosoa
viongozi pale wanapokengeuka.
“Nyimbo zenye soko ni zile za kukosoa mabaya ya watu
Fulani lakini changamoto ni kwamba watu wa tabaka la juu wao hutaka nyimbo za
kusifia tu” amesema Msanii huyo
Hivyo amesema waziri mwenye dhamana anatkiwa
ahakikishe uhuru wa wasanii ili kufanya kazi kwa mapana zitakazogusa maisha
halisi ya wazanzibar.
“Waziri mwenye dhamana atuhakikishie uhuru na
usalama wetu ili tufanye kazi zenye kuibua changamoto na kadhia za wananchi”
amemalizia
Hata hivyo wasanii hao wamesema wanalazimika kutoa
maudhui ya jamii nyingine na kuziacha jamii zao ambazo zina mikasa mingi ya
kusisimua ambayo inahitajika kutolewa maudhui.
0 Comments