Picha Kwa Msaada wa DW |
NA Ahmed Abdulla:
Licha ya sauti zinazopazwa na wadau mbalimbali
ikiwemo chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania Tamwa-Zanzibar pamoja
na Internews kuhusu uwepo wa uhuru wa kujieleza kwa makundi mbalimbali lakini
bado makundi mengi kiuhalisia yananyimwa uhuru wa kujieleza na makundi
minginekutokana na mfumo wa sheria kuyapa nguvu makundi hayo.
Miongoni mwa kundi lisilo na uhuru wa kujieleza
mbele ya wengine ni waandishi wa habari ambapo mifano mingi inaonyesha
waandishi wa habari kunyimwa uhuru katika utekelezaji wa majukumu yao.
Mfano mdogo tu ni ule wa mwandishi wa habari wa
gazeti la Mwananchi Jessy Mikofu kupata manyanyaso kutoka vikosi vya SMZ
vilipokuwa vikifanya majukumu yao ya kuwatawanya wafanyabiasha wadogo wadogo
waliokuwa hawapo kisheria.
Huo ni mfano unaoonyesha waandishi kunyimwa uhuru wa
kutekeleza majukumu yao hali inayoleta hofu kwa waandishi kuibua mambo mazito
kwa maslahi ya taifa.
Hilo lilikuwa ni jicho la Zanlight Blog lakini
tulifunga safari kuwafata waandishi wenyewe jee wanasemaje kuhusu uhuru wao.
Omar Abdulla ni muandishi wa habari wa East Afrika
TV kwa upande a Zanzibar yeye anasema uhuru uliokuwepo ni wa kusifia watu wa
jamii Fulani tu lakini ukiamua kufatilia mapungufu yao unaanza kupokea vitisho
hali inayowapunguza ari ya ufautiliji wa mambo mbalimbali.
“Thuru tulionao ni wa kusifia tu na si wa kukosoa
tunapokosoa tunakuwa ni waja wa kupokea vitisho tu” alisema Omar
Amesema katika kutafuta mwarobaini wa hilo kuna kila
sababu ya kuangalia upya nguvu zilizotolewa kwa baadhi ya makundi na uhuru wa
waandishi wa habar.
“Tunahitaji uhuru wetu ulioainishwa kwenye sheria
uheshimiwe na makundi yote na wao pia wapunguziwe nguvu walizopewa” aliongezea
Dhulkaada Khamis kutoka Zenj Online TV ameseama ndio
kwanza anaingia kwenye tasnia ya habari lakini ana hofu ya kuandika habari za
uchunguzi kwani hao waliomtangulia nao pia anahisi wanahofu.
Amesema ili kuisaidia serikali katika kuibua mambo
mbalimbali basi waandishi wanatakiwa kuwa na uhuru wa kweli kwani kwa sasa
uhuru wao ni kama umezuiwa na makundi mingine.
“Tunaambiwa tuna uhuru lakini ninavyoona uhuru wetu
umeporwa tuachiwe tisaidie serikali yetu” alisema Dhulkaada
Kwa upande wake Kher Abdulqadir Kheir ambaye ni
muandishi wa habari wa kujitegemea amesema kwa miaka mitano iliyopo uhuru wa
vyombo vya habari ulianza kupotea japo wanapambana kuona wanapata sheria bora
zitakazowapatia uhuru wa kweli.
Aidha amesema kwa muandishi mwenyewe ndio uhuru
umekosekana kabisa kwani hata anapoandaa habari yenye kuonyesha madhaifu ya
watu wa tabaka fulani basi kuna uwezekano wa habari hiyo isitolewe na Mhariri
wa chombo cha habari kwa horu ya kufungiwa chombo cha habari hicho.
"Kwa muandishi wa habari ndio kwenye tatizo
zaidi kwana anaweza kuandaa habari yake lakini mhariri akaikataa kwa kuhofia
kufungiwa chombo chao cha habari" Amesema Kher Abdulqadir
Kulingana na waliyoyazungumza waandishi wa habari na
mfano tulioutoa hapo juu basi kuna sababu kwa Serikali kuweka sheria itakayotoa
uhuru wa kweli kwa waandishi wa habari na vyombo vya habari ili kuona sekta
hiyo inaisadia serikali kuibua changamoto katika sekta mbalimbali za umma kwa
lengo la kufikia maendeleo ya kweli.
0 Comments