Na Ahmed Abdalla
Kwa
miaka mingi watalamu na wadadisi mbali mbali ulimwemguni kote wamediriki kusema
hakuna jamii yoyote hile inayoweza kupiga hatua kimaendeleo iwapo wananchi wake
hawatakua na uhuru wa kujieleza na kutoa maoni yao.
Kwa
minajili hii tunaaminishwa na kuamini kuwa uhuru wa kujieleza ni nguzo muhimu
ya kusukuma maendeleo mdami ya Nchi yoyoter hile.
Visiwani
Zanzibar inaendelea kuaminika kuwa hadi sasa bado haki hii ya kujieleza imekua
ikakandamizwa kwa kiasi Fulani kupitia sharia ya habari ya mwaka 1988.
Licha
ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano Tanzania na hile ya Zanzibar kuweka wazi haki
hio ya kujieleza lakini bado sharia nyengine zimekua zikikandamiza na ndio
maana wadau wa habari visiwani hapa wanaeleza kuwa haki hiyo imetolewa kwa
mkono wa kulia na kunyanganywa kwa mkono wa kushoto.
Kutokana
na uwepo wa mazingira hayo Chama cha waandishi wa habari wanawake TAMWA-ZNZ kwa
kushirikiana na Internews Tanzania wanaendelea na mradi maalumu wa
kuwakutanisha wanahabari kutazama na kujadili kwa pamoja sharia hiyo ya habari
na kasha kutoa mapendekezo yao ili yaingizwe kwenye sharia mpya ya habari
inayosubiriwa kwa hamu visiwani hapa.
Wakiwa
katika majadiliano ya kupitia sharia hiyo baadhi ya waandishi wa habari
visiwani hapa walionesha miongoni mwa sehemu ambazo wanaamini kuwa zinanyima
uhuru wa kujieleza sambmba na uhuru wa habari kiujumla.
Kwa
mfano moja miongoni mwa vipengele vya sharia hiyo kinasema Kifungu cha 27 (2)
Hakimu yeyote anaweza kutoa hati kumuidhinisha afisa polisi yeyote wa cheo cha
Inspekta, kwa msaada au bila msaada kuingia na kupekua mahali popote pale
ambapo inashukiwa kuwa kuna gazeti linachapishwa kinyume na Sheria hii
linafanya kosa chini ya Sheria hii au
kanuni zozote zilizotungwa ama limefanya, linafanya au linakaribia kufanya
kosa, hivyo anaweza kukamata.
Miongoni mwa
washiriki walisema kitendo cha sharia hiyo kulipa mamlaka makubwa jeshi la
polisi ni kukandamiza uhuru wa habari na uhuru binafsi wa mtu kujieleza na sharia
hiyo inapaswa kubadilishwa ili kuendana na wakati tuliona.
Juma Khamis alisema
anaamini iwapo mazingira bora na sharia imara itakapokamilika Zanzibar itapiga
hatua kubwa zaidi za kimaendeleo na kuwa mfano duniani kote.
Issa Yussuf alisema
licha ya uwepo wa changamoto hizo lakini kuna haja ya wanahabari kutambua sharia
wanazozifanyia kazi kila leo ili kujiweka katika mazingira salama muda wote.
Awali mkurugenzi wa
TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa alisema wanahabari wanawajibu mkubwa kuhakikisha
Zanzibar inapata sharia bora ya habari kwa maslahi mapana ya tasnia na Taifa
kwa ujumla.
Alisema sharia iliopo
sasa ya habari haiendani na wakati tulionao na hwenda ilitungwa katika kipindi
ambacho wengi waliokua hawajaona umuhimu wa mambo mengi ambayo sasa
yamejitokeza hivyo kuendelea kuyawekea sharia ngumu ni kunyima uhuru wa walio
wengi ambao nao pia wanapaswa kusikilizwa.
0 Comments