Na Ahmed Abdalla
Imelezwa kuwa haki ya
uhuru wa kujieleza ni miongoni mwa haki muhimu katika jamii ambayo ikitekelezwa
ipasavyo inachangia kwa kiasi kikubwa kuibadili jamii katika nyanja mbali
mbali.
Kauli hiyo imetolewa na
mkuu wa miradi kutoka TAMWA-ZNZ Ali Mohamed wakati alipokua akifungua mkutano
maalumu wa majadiliano kuhusu umuhimu wa haki ya kujieleza na uhuru wa habari.
Amesema iwapo jamii
itajengewa misingi imara ya kutumia haki hiyo ni wazi kuwa kutajengwa jamii bora
yenye kuleta usawa kwa kila nyanja.
Alisema kupitia mradi
huo unaofanywa na TAMWA-ZNZ kwa mashirikiano na Intaernews Tanzania unalengo la
kuwakumbusha wanahabari kuhusu umuhimu wa haki ya kujieleza na kutoa fursa
zaidi kwa jamii ili waweze kupaza sauti zao.
Awali wakichangia
majadiliano hayo baadhi ya waandishi wa habari walisema kuna changamoto katika
upatikanaji wa haki hiyo ukizingatia baadhi ya wanajamii hawafahamu kama ni
haki yao ya kikatiba.
Issa Yussuf ambae ni
mwakilishi kutoka gazeti la Daylnews alisema licha ya hali hiyo lakini baadhi
ya wanahabari nao hawafahamu umuhimu wa haki ya kujieleza na ndio maana wamekua
wakiwanyima walio wengi fursa kupitia vyombo vyao vya habari.
Nae Juma Khamis kutoka
shirika la magazeti ya Serikali Zanzibar alisema mafanikio yoyote yale kwenye
jamii hayawezi kujitokeza pasi na kuwepo kwa uhuru wa habari na kwamba ili
tuweze kuendelea ni lazima Nchi iwe na uhuru wa habari wenye kuheshimiwa.
Pia alisema vyombo vya
habari vinawajibu wa kutambua kutoa fursa kwa jamii kupaza sauti zao hakuvunji
uhuru wala kanuni za habari badala yake ni kuwatendea haki wananchi wasiokua na
sauti.
Wakitaja baadhi ya
changamoto walisema walisema wanahabari wengi na jamii kwa ujumla wamejawa na
hofu na ndio maana hata wao wenyewe hushindwa kuandika au kuripoti baadhi ya
habari wanapoona zinawagusa baadhi ya watu.
Sambamba na hayo
walisema kutokana na dhana ya hofu iliowajaa wananchi na wanahabari wenyewe
wana wajibu wa kuhakikisha kuwa wanajenga jamii huru yenye uwezo wa kusema
mapungufu wanayoyaona kila leo.
Kwa upade wake mratibu
wa mradi huo Muhammed Khamis alisema mradi huo unatekelezwa na TAMWA-ZNZ kwa
kushirikiana na Internews Tanzania wenye lengo la kupitia sheria ya habari sambamba na kujadili mazingira ya kazi katika
tasnia ya habari visiwani Zanzibar.
Alisema kuna umuhimu
mkubwa wa watu kupata haki ya kujieleza ukizingatia kuwaweka watu huru
huchochea upatikanaji wa maendeleo katioka Taifa lolote ulimwenguni.
0 Comments