Na Ahmed Abdulla Othman
NAIBU Katibu mkuu Wizara ya
habari Zanzibar Khamis Said amesema wakati umefika wa sheria ya habari Zanzibar
kufanyiwa marekebisho kwa kuwa sheria inayotumiwa sasa imekua na changamoto
mbalimbali ambazo ni kikwazo kiutendaji.
Aliyasema hayo katika
mkutano maalumu uliowashirikisha wajumbe wa kamati ya ustawi wa jamii ya Baraza
la wawakilishi na maafisa mbalimbali wa Serikali ulioandaliwa na TAMWA-ZNZ kwa kushirikiana na
Internews Tanzania.
Alisema kwa miaka mingi
Zanzibar imekua ikitumia sheria hio ya habari ambayo kwa mazingira yaliopo sasa
haiendani na wakati na kwamba Serikali kupitia Raisi Mwinyi imeshafungua milango
ya wadau kutoa maoni juu ya mabadiliko ya sheria hiyo.
Sambamba na hayo alisema
wadau wana wajibu wa kujadili na kutoa maoni pale wanapoona kuna changamoto za
kisheria ili Serikali iweze kuzifanyia kazi.
Kwa upande wake Mwenyekiti
wa kamati ya ustawi wa jamii ya Baraza la wawakilishi Mohamed Ahmada alisema
wao kama wajumbe wamepata wakati mzuri wa kufanyiwa mafunzo hayo ambayo kwa
kiasi kikubwa yamewajengea uwezo.
Alisema kwa kuwa Baraza la
Wawakilishi linawajibu wa kujua sheria nyingi ili waone mapungufu ya sheria
hizo hatimae waongeze nguvu katika kutetea mabadiliko ya sheria mpya.
Alisema kupitia mafunzo
hayo waliopatiwa na TAMWA-ZNZ kwa kushirikiana na Intenrnews yamefungua na
kuwafanya wawe na uelewa mpana kuhusu sheria ya habari inayoendelea kutumika
hadi sasa Zanzibar.
Alisema mara baada ya
kupatiwa elimu hio watahakikisha mswaada wa sheria hio utakapopelekekwa Baraza
la wawakilishi watajenga hoja imara ambazo zitasaidia kuwaeleza wajumbe wengine
umuhimu wa sheria mpya ya habari.
Kwa upande wake Mkurugenzi
wa TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa alisema haki ya kupata habari ni haki ya kikatiba
ambayo inapaswa kuheshimiwa na kila mmoja.
Alisema si sahihi kuona
hadi leo hii licha ya kuwa kupatikana kwa habari ni haki ya kikatiba lakini
ikawa inakinzana na sheria ambazo zimewekwa kupitia sheria ya habari.
Alisema sekta ya habari ni
muhimu na chanzo cha maendeleo na kufungua fursa zaidi kimataifa hivyo inapaswa
kuwa huru na kuheshimiwa.
0 Comments